"Sijaoa kwa sababu sijapata mke mcha Mungu, mwenye hapendi mitandao ya kijamii" - Sadio Mane

Mchezaji huyo alisema mwanamke atakayemuoa sharti awe mcha Mungu na pia asiwe mwenye uraibu wa mitandao ya kijamii

Muhtasari

• “Nimeona wasichana wengi wakiniuliza kwa nini sijaoa. Nataka kuoa mwanamke anayemheshimu Mungu na anayesali vizuri.”

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Senegal, Sadio Mane
Image: Frank Khalid (Twitter)

Je, unafahamu ni kwa nini mpqaka sasa mwanasoka maarufu kutoka Senegal, Sadio Mane hajaoa?

Kama ulikuwa hujui basi habari ndio hiyo kwamba mchezaji huyo matata mwenye umri wa miaka 30 hadi sasa licha ya kubarikiwa na kipaji na utajiri pia bali hajapata kuoa kwa sababu zake za kibinafsi tu.

Katika mahojiano ya kipekee na mfanyibiashara ambaye pia anajiongeza kama mfuatiliaji mkubwa wa mchezo wa soka, bwana Frank Khalid, Sadio Mane alikiri kwamba hajawahi oa na wala hajakuwa na mpango wa kuoa kwa sababu hajamuona mwanamke mwenye vigezo anavyovitaka yeye.

Mchezaji huyo alisema kwamba kigezo kikubwa atakachokiangalia kwa mpenziwe ni kuwa asiwe mwanamke uraibu wa mitandao ya kijamii kwa maana ya Facebook, Twitter, Instagram, Skype, TiktTok miongoni mwa mitandao mingine.

Kutokana na utandawazi ambao umewavutia wanawake wengi tu kutaka kujumuika kwenye makundi ya mitandaoni, basi hili limefanya kuwa vigumu kwa Mane kumpata mchumba. Kando na kigezo hicho, pia Mane alisema mchumba wake sharti awe mcha Mungu.

“Nimeona wasichana wengi wakiniuliza kwa nini sijaoa, lakini samahani unaweza kuwa unapoteza muda wako. Mwanamke nitakayemuoa hatakuwepo kwenye mitandao ya kijamii (Tik Tok, Facebook, Instagram, Twitter) nataka kuoa mwanamke anayemheshimu Mungu na anayesali vizuri.” Aliandika mchambuzi wa soka Frank Khalid kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Sadio Mane wiki jana alitangaza kuigura timu ya Liverpool baada ya kutumikia miamba hao wa Uingereza kwa muda wa miaka 6 na kujiunga na Bayern Munichen ya Ujerumani kwa kandarasi ya miaka mitatu.

Katika ujumbe wake wa mwisho kwa mashabiki wa timu hiyo ya Anfield, Mane alisema kwamba Liverpool ilifanya jina lake kuheshimika baada ya kushinda mataji mbalimbali ya ndani na nje ya Uingereza na timu hiyo na kuahidi kwamba siku zote atabaki kuwa shabiki namba moja wa Liverpool hata baada ya kuondoka kwake.

Katika kipindi cha miaka sita, Mane alisaidia Liverpool kushinda mataji kama vile taji la Carabao, Taji la ligi kuu ya premia, Taji la ubingwa wa Uropa miongoni mwa mataji mengine. Pia alishinda taji la kuwa mfungaji bora wa msimu.