Paul Pogba ajiunga tena na Juventus baada ya miaka 6

Amejiunga kwa uhamisho wa bila malipo baada ya mkataba wake Manchester United kumalizika.

Muhtasari

•Pogba alisafiri kwa ndege hadi Turin siku ya Ijumaa kwa ajili ya vipimo vya matibabu kabla ya kutangazwa ramsi Jumatatu.

•United na Pogba hawakuweza kuafikiana kuhusu mkataba mpya na klabu hiyo ilithibitisha kwamba angeondoka kama mchezaji huru.

Image: BBC

Paul Pogba amejiunga tena na Juventus kwa uhamisho wa bila malipo baada ya mkataba wake Manchester United kumalizika.

Kiungo huyo wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 29 alishinda taji la Serie A mara mbili na miamba hao wa Italia kabla ya uhamisho wa rekodi ya dunia wa £89m kwenda United mwaka 2016.

Alisafiri kwa ndege hadi Turin siku ya Ijumaa kwa matibabu yake kabla ya kutangazwa ramsi Jumatatu.

Pogba hakuwa ameichezea United tangu Aprili baada ya kusumbuliwa na jeraha.

Juventusi alisema: "Tunapoagana baada ya tukio kubwa lililoshirikiwa pamoja, daima kuna matumaini kwamba tutaonana tena, mapema au baadaye.

"Aliondoka akiwa mvulana na anarudi kama mwanamume na bingwa, lakini kuna jambo moja ambalo halijabadilika - hamu ya kuandika kurasa zisizosahaulika za historia ya klabu kwa mara nyingine tena. Pogba amerejea na hatukuweza kuficha furaha."

United na Pogba hawakuweza kuafikiana kuhusu mkataba mpya na klabu hiyo ilithibitisha mwanzoni mwa Juni kwamba ataondoka kama mchezaji huru msimu huu wa joto.

Pogba alijiunga na akademi ya United kutoka Le Havre.