RIP! Aliyekuwa kiungo wa kati wa Sofapaka Naya, afariki kwa kansa akiwa na miaka 19

Wisdoma alipata mkataba na Sofapaka baada ya kufana katika fainali za ubingwa wa mataifa ya Afrika walipoinyuka Nigeria kwenye penati.

Muhtasari

• Umaarufu wake uling'aa pale alipoitumikia St. Anthony ya Kitale iliyowakilisha Kenya kwenye mashindani ya taifa bingwa Afrika dhidi ya Nigeria.

• Sofapaka walimpa mkataba akiwa na umri wa miaka 16.

Aliyekuwa kiungo wa kati wa timu ya Sofqapaka, kinda Wisdom Nayah katika pambano la awali uwanjani.
Aliyekuwa kiungo wa kati wa timu ya Sofqapaka, kinda Wisdom Nayah katika pambano la awali uwanjani.
Image: Twitter

Aliyekuwa mchezaji wa kiungo cha kati wa timu ya soka ya Sofapaka Wisdom Naya amefariki dunia baada ya vita vya muda mrefu na ugongwa wa saratani.

Mchezaji huyo kinda mwenye miaka 19, alipatikana na kansa miaka michache tu baada ya kuanza safari yake ya kucheza soka ya kulipwa, tatizo ambalo lilisababisha yeye kukatwa mguu wake wa kushoto.

Kifo cha mchezaji huyo kinda kilitangazwa Ijumaa asubuhi na wadau katika soka ya Kenya ambapo wengi wamemuomboleza kama kijana ambaye nyota yake ilizimwa pindi tu ilipoanza kung’aa.

“Ghafla tumempoteza kiungo wetu wa zamani Wisdom Naya. Kijana huyo amefariki kutokana na tishu laini, Sarcoma. Pole zetu za dhati kwa familia na marafiki wa Naya. Apumzike pema,” taarifa kutoka klabu ya Sofapaka ilichapishwa kwenye ukurqasa wao wa Facebook.

Naya alipata umaarufu baada ya kuifikisha timu ya soka ya shule ya upili ya Wavulana St. Anthony Kitale kwenye fainali za Copa-CocaCola mwaka wa 2015 kipindi akiwa mwanafunzi shuleni humo. Fainali hizo zilikuwa za ubingwa wa mataifa ya bara la Afrika ambapo kikosi chao kiliwanyuka Nigeria mikwaju ya penati 4-3 ambapo aling’aa sana na kupata mkataba kuitumikia Sofapaka akiwa na umri wa miaka 16 tu.

Baadae alipopata jerqaha uwanjani ndio matatizo yake yalianza ambapo alilazwa katika hospitali mbali mbali na Januari mwaka huu washika dau mbalimbali walijumuika na kuandaa kipute cha soka kwa ajili ya kuchangisha hela za matibabu yake India kukatwa mguu huo baada ya kupatikana na aina ya kansa hiyo adimu.