Sadio Mane awabwaga Salah na Mendy kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka CAF

Mchezaji huyo aliihama Liverpool mwishoni mwa msimu jana na kujiunga na Bayern Munich ya Ujerumani.

Muhtasari

• Mane aliisaidia timu ya taifa ya Senegal kushinda kombe la ubingwa wa Afrika CAF  kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo.

Mchezaji wa kimataifa wa Senegal na timu ya Ujerumani Bayern Munich
Mchezaji wa kimataifa wa Senegal na timu ya Ujerumani Bayern Munich
Image: BBC

Kama kuna watu ambao wanafaa kupiga goti na kusali kutokana na huu mwaka kuwa mzuri wenye baraka tele kwao basi si mwingine bali ni mchezaji wqa kimataifa wa Senegali, Sadio Mane.

Hii ni baada ya msanii huyo kwa mara nyingine tena kutangazwa mshindi wa tuzo za CAF usiku wa kuamkia leo.

 Hafla ya tuzo hizo za CAF ziliandaliwa katika jiji la Rabat nchini Morocco ambapo Sadio Mane wa Bayern Munichen alitangazwa mshindi katika kitengo cha mchezaji bora wa mwaka, kitengo ambacho alikuwa akimenyana na mchezaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri, Mohammed Salah na golikipa wa Chelsea na timu ya taifa ya Senegali, Edouard Mendy.

Bila shaka ushindi huu wa Mane si wa kubahatisha kwani matokeo yake yameonekana ya kufana tangu mwaka jana akiisakatia Liverpool kabla ya kuondoka Kwenda Ujerumani kujiunga na miamba ya BundesLiga, Bayern Munichen katika uhamisho wa msimu huu wa joto.

Akiwa Liverpool, Mane alisaidia timu hiyo kushinda mataji ya Carabao na FA msimu jana na pia kuisaidia timu hiyo ya Uingereza kufika kwenye fainali za kombe la klabu bingwa barani Uropa.

Kando na hapo, Mane pia aliisaidia timu yake ya taifa ambapo pia anawakilisha kama nahodha kushinda kombe la ubingwa wa Afrika, CAF kwa mara ya kwanza kabisa baada ya kufunga penati ya ushindi katika mchuano wa fainali uliowakutanisha na mchezaji mwenza kipindi hicho katika timu ya Liverpool, Mohammed Salah.

Kama hiyo haitoshi, watani hao wawili tena walikutana katika mechi ya kufuzu kushiriki ngarambe ya kombe la dunia inayoanza Novemba nchini Qatar ambapo kwa mara nyingine tena Mane alifana katika mchezo huo na kuisaidia Senegali kufuzu kwa kuishinda Misri.

Baada ya miaka zaidi ya mitano akiisakatia Liverpool, Mane alitangaza kugura timu hiyo mwezi mwishoni mwa mwezi jana na kujiunga na Bayern Munich ambapo tayari ashaanza kujijengea heshima yake katika mioyo ya mashabiki wa timu hiyo ya Ujerumani baada ya kufunga bao lake la kwanza katika mechi ya kujipima nguvu ambapo walishinda mabao sita kwa nunge.