logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Chelsea na Barcelona waanza mazungumzo ya kumnunua Frenkie de Jong

Kiungo mahiri, anasifika kwa pasi, chenga, ufundi wake wa kandanda uwanjani pamoja na uwezo mkubwa wa ulinzi na umahiri wa kushambulia.

image
na Radio Jambo

Habari03 August 2022 - 05:00

Muhtasari


•Baada ya kutangaza nia yao mwishoni mwa wiki, Chelsea sasa wamefungua mazungumzo rasmi na Barcelona.

 

Mwanasoka Frenkie De Jong

Imeonekana wazi kuwa Barcelona wako tayari kumuuza Frenkie de Jong kwa klabu ya Chelsea uendapo wanaweza kutimiza matakwa yao.

Manchester United ndiyo ilikuwa timu pekee iliyoonyesha nia ya dhati kwa de Jong, lakini Chelsea sasa wana kibali cha meneja Thomas Tuchel kuanzisha mazungumzo ya kumnunua de Jong.

Baada ya kutangaza nia yao mwishoni mwa wiki, Chelsea sasa wamefungua mazungumzo rasmi na Barcelona.

Klabu ya Barcelona wanataka angalau  pauni 80m kwa de Jong, sio siri kuwa Barcelona pia wana nia ya kuwanunua wachezaji wa Chelsea Marcos Alonso na Cesar Azpilicueta, jambo ambalo Wanablues wanatumai kuwa litawasaidia katika mazungumzo.

Joan Laporta hatakubali kujumuishwa moja kwa moja kwenye dili la de Jong, kwani hilo litakuwa na manufaa kidogo kwao katika suala la kukidhi viwango vya mishahara ya La Liga.

Ikiwa Chelsea inaweza kukidhi matakwa ya Barcelona, ​​basi itabidi wafanikiwe pale United ilishindwa kuafikiana na Barcelona.

Tuchel bado lazima amshawishi de Jong kuungana na klabu ya Chelsea, kwani uamuzi huo itasaidia Chelsea inaweza kubeba taji ya Ligi ya Mabingwa.

Frenkie de Jong ni mchezaji wa soka wa Uholanzi ambaye anacheza kama kiungo wa klabu ya La Liga ya Barcelona na timu ya taifa ya Uholanzi.

Kiungo mahiri, anasifika kwa pasi, chenga, ufundi wake wa kandanda uwanjani pamoja na uwezo mkubwa wa ulinzi na umahiri wa kushambulia.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved