logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Christiano na Maguire wanaongoza kwa orodha ya wachezaji waliodhulumiwa mitandaoni

Twiti za matusi pia zilipatikana kuwaathiri wachezaji saba kati ya 10 wa ngazi za juu.

image
na Radio Jambo

Burudani03 August 2022 - 09:05

Muhtasari


•Angalau posti 60,000 za matusi zilipatikana zikielekezwa kwa wachezaji wa Ligi Kuu, na zote zilisambazwa katika msimu wa 2021/22.

 

Harry Maguire na Cristiano Ronaldo wakati wa mechi.

Cristiano Ronaldo na Harry Maguire ndio wachezaji wanaonyanyaswa zaidi kwenye Twitter kwa njia ya matusi, kulingana na utafiti mpya.

Utafiti huo ulifanywa na Ofcom na Taasisi ya Alan Turing ya nchini Uingereza, na iligundua kuwa Ronaldo, licha ya kuwa mfungaji bora wa Manchester United msimu uliopita akiwa na mabao 24, alipata dhuluma nyingi zaidi kwenye Twitter.

Angalau posti 60,000 za matusi zilipatikana zikielekezwa kwa wachezaji wa Ligi Kuu, na zote zilisambazwa katika msimu wa 2021/22.

Ronaldo alitumiwa ujumbe mwingi zaidi wa matusi kuanzia Agosti 13 na Januari 24, huku ujumbe mwingi 12,520 ukiwa na lengo la kumkashifu mshindi huyo mara tano wa Ballon d’or.

Nahodha wa United Harry Maguire alishika nafasi ya pili kwenye orodha hiyo, akiwa na angalau jumbe 8,954 za matusi zilizoelekezwa kwake katika kipindi hicho.

Twiti za matusi pia zilipatikana kuwaathiri wachezaji saba kati ya 10 wa ngazi za juu.

Wachezaji wengine waliokuwa kwenye 10 bora ya waliodhulumiwa zaidi mtandaoni ni pamoja na Marcus Rashford (2,557), Bruno Fernandes (2,464), Fred (1,924), Jesse Lingard (1,605), Paul Pogba (1,446) na David De Gea (1,394), wote kutoka Manchester United.

Harry Kane (2,127) na Jack Grealish (1,538) pia wameingia kwenye orodha hiyo.

Hivi karibuni, Cristiano Ronaldo amekuwa na ushirikiano mbaya na mashabiki wa Manchester United baada ya kueleza nia yake ya kutaka kuihama klabu hiyo.

Hata hivyo, baada ya kushindwa kupata klabu inayofaa kwenye Ligi ya Mabingwa, Ronaldo alirejea katika klabu hiyo na kushiriki mechi ya kirafiki dhidi ya Rayo Vallecano Jumapili, Julai 31.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved