Aubameyang kujiunga na Chelsea, Barcelona wako tayari kumuuza

Barcelona wako tayari kumuuza mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 33, kwenda Chelsea

Muhtasari

Wakati huohuo Ombi la Chelsea la kutaka kumnunua mlinzi wa Leicester Wesley Fofana,21,  kwa pauni milioni 60 limekataliwa.. (Mail)

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Pierre Emeric Aubameyang
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Pierre Emeric Aubameyang
Image: GETTY IMAGES

Barcelona wako tayari kumuuza mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 33, kwenda Chelsea. (Mirror)

Wakati huohuo Ombi la Chelsea la kutaka kumnunua mlinzi wa Leicester Wesley Fofana,21,  kwa pauni milioni 60 limekataliwa.. (Mail)

The Blues sasa wanafikiria kutoa ofa iliyoboreshwa ya dau la £70m kwa Fofana. (Times - subscription required)

Nottingham Forest wameanza mazungumzo na Southampton kuhusu kumsajili mshambuliaji wa Scotland Che Adams, 26. (Football Insider)

Wesley Fofana
Wesley Fofana

Forest pia wanavutiwa na kiungo wa kati wa Wolves Muingereza Morgan Gibbs-White, 22. (Sky Sports)

Tottenham wanakaribia kufikia makubaliano ya pauni milioni 21 kumnunua beki wa kushoto wa Udinese wa Italia mwenye umri wa miaka 19, Destiny Udogie (Telegraph)

Maxwel Cornet wa Burnley, 25, anatazamiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu huko West Ham baada ya kuafikia kipengele cha kumnunua  winga huyo wa Ivory Coast cha pauni milioni 17.5. (Mail)

Manchester United wako tayari kujiondoa kwenye vita vya kuwania saini ya kiungo wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong dhidi ya Chelsea,25. (Mirror)

Frankie de Jong
Frankie de Jong
Image: GETTY IMAGES

Lucas Torreira amekubali kujiunga na Galatasaray, ambayo itailipa Arsenal kati ya dau la £5m na £6m kumnunua kiungo huyo wa Uruguay, 26. (Fabrizio Romano)

Juventus are keen on a deal to sign Netherlands forward Memphis Depay, 28, from Barcelona. (Sport - in Spanish)

Real Madrid inatumai klabu ya Nice itapunguza thamani yao ya euro 40m (£33.7m) kwa Amine Gouiri ili waweze kumsajili mshambuliaji huyo wa Ufaransa, 22, kwa nia ya kusalia na timu hiyo ya Ufaransa kwa mkopo msimu huu. (Sport - in Spanish)

Kocha mpya wa Paris St-Germain Christophe Galtier anatumai kusajili wachezaji wengine watatu baada ya kiungo wa kati wa Ureno Renato Sanches, 24, kujiunga nao kutoka Lille na kuwa mchezaji wao wa nne kusajiliwa majira ya kiangazi. (Sport - in Spanish).

GETTY IMAGES Maelezo ya picha, Memphis Depay
GETTY IMAGES Maelezo ya picha, Memphis Depay
Image: GETTY IMAGES

Beki wa kushoto wa Uhispania Angelino anakaribia kujiunga na Hoffenheim kwa mkopo kutoka RB Leipzig, licha ya Brighton, Barcelona na Sevilla pia kumtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (AS - in Spanish)

Klabu ya Charlotte FC katika ligi ya Marekani ya  MLS wanakamilisha dili la kumsaini beki wa pembeni wa Uingereza Nathan Byrne, 30, kutoka League One Derby County. (90min).