Sadio Mane akataa kupiga picha na pombe, sheria za dini ya Kiislamu haziruhusu!

Mane aliketishwa mbele, huku Mazraoui akisimama karibu na Jamal Musala katika safu ya tatu.

Muhtasari

• Jumla ya watu 31 wanaojumuishwa na wachezaji na wafanyakazi walijitokeza kwenye picha

Mchezaji Sadio Mane akataa kushikilia pombe wakakti wa picha ili kuheshimu sheria za dini ya kiislamu
Mchezaji Sadio Mane akataa kushikilia pombe wakakti wa picha ili kuheshimu sheria za dini ya kiislamu
Image: Facebook//Bayern Munich

Dini ya Kiislamu ni moja ya dini zenye utaratibu wa aina yake katika kufanya mambo mbali mbali, taratibu ambazo zinapigigwa mifano ya kuigwa.

Jana, klabu ya Bayern Munich ilikuwa inasherehekea kuingia mkataba na moja ya kampuni ya kutengeneza mivinyo nchini Ujerumani ambapo wachezaji wote walijumuika na kupigwa picha ya pamoja wakiwa wameshikilia gilasi ya pombe hiyo.

Jumla ya watu 31 wanaojumuishwa na wachezaji na wafanyakazi walijitokeza kwenye picha lakini wawili tu hawakuwa na bia mkononi - Mane na mchezaji mwenzake mpya aliyesajiliwa Noussair Mazraoui, raia wa Morocco.

Wote wawili ni Waislamu waaminifu na unywaji wa pombe ni haramu katika Uislamu. Wawili hao bado walikuwa na tabasamu na wanapaswa kupongezwa kwa kufanya juhudi ya kuzama katika utamaduni wa Bavaria.

Mane aliketishwa mbele, huku Mazraoui akisimama karibu na Jamal Musala katika safu ya tatu.

Mane ambaye ni mkereketwa wa dini ya Kiislamu ana Imani kubwa kwamba vileo vya aina yoyote ni haramu kulingana na mafunzo ya dini hiyo na ndio maana alijitenga kabisa na kushika gilasi yenye kileo hicho.

Itakumbukwa mwenzi Februari mwaka huu timu ya Liverpool iliposhinda taji la Carabao, wachezaji walisherehekea huku video ikiibuka ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegali akimkanya vikali mchezaji mwenza Takumi Minamino dhidi ya kummiminia kileo kimoja waakti wa kusherehekea.

Hii si mara ya kwanza kwa wanaimani ya Kiislamu kujitenga kabisa na vileo kulingana na mafunzo ya dini hiyo kwani mwaka jana pia palizuka habari nchini Tanzania kwamba mwanamuziki nguli malkia wa Bongo Fleva Zuchu akifuatwa na kampuni maarufu ya vileo waliotaka kumpa mkataba wa kuwa balozi wa mauzo ya bidhaa zao ila akakataa licha ya kuahidiwa kima kirefu cha fedha.