(+video) Mchezaji atokwa na kaptura aking'ang'ania mpira na mpinzani

Hakufa moyo kwani alijikusanya na kujivalisha kaptura kabla ya kuuwahi mpira ule tena.

Muhtasari

• Alionekana fikira zake zote kazielekeza kwenye mpira licha ya kaptura kumtoroka.

Katika michezo siku hizo kwenye ulingo wa kandanda, au hata riadha, pametokeoa matukio yasiyo ya kawaida ambapo washiriki katika mashindano wamekuwa wakionekana kuwa na kuchanika kwa nguo na kuishia kuonesha nyeti zao kwa mashabiki pasi na kutaka kwao.

Hali ni sawa katika klipu moja ambayo imekuwa ikipakiwa kweney mitandao ya kijamii haswa Twitter Jumatano ikimuonesha mchezaji mmoja wa soka akipukutika chini na kaptura kumtoka.

Mchezaji huyo hata hivyo hakufa moyo kwani alijikusanya na kuamka kuendelea na mchezo huku akiivuta kaptura juu kwa haraka mno pasi na kujali kile watu wameona. Mchezaji huyo alionekana kuhusika katika mzozo mkali wa kupiga mpira na mpinzani wakati kaptura yake iliteleza kutoka kwa goti lake wakati anaanguka chini.

Alionekana fikira zake zote kazielekeza kwenye mpira.

Kilichochekesha zaidi ni pale anaamka na kuuwahi mpira tena na kuucheza mbele huku akiivaa vizuri kaptura ile na mchezo kuendelea bila kipenga kupulizwa na refa.

Video hiyo ilipakiwa kwenye ukurasa wa Twitter unaokusanya na kupakia matukio ya kuchekesha katika mchezo wa soka ila haukumtambua mchezaji huyo ni nani na alikuwa anaiwakilisha timu gani.

Tukio la wachezaji kupukutikwa na kaptura mchezoni si la kwanza kutokea kwani itakumbukwa pia mwaka 2013 wakati wa kipute cha Carabao, mshambuliaji wa Aston Villa Nicklas Helenius alivuliwa suruali na beki wa Tottenham Jan Veetonghen.

Pia wiki chache zilizopita kinda wa riadha kutoka Italia alikuwa mbioni wakati uume wake ulitokelezea kwa kaptura na kulemaza kasi yake ambapo alimaliza wa mwisho kweney mashindano hayo.