logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kampuni ya filamu za watu wazima yatoa ombi la kutaka kuitwa jina la uwanja mpya wa Everton

Stripchat wamezindua ofa ya pauni milioni 180 wakitaka kupewa haki za kuitwa jina la uwanja wa Everton - Daily Mail waliripoti.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri08 October 2022 - 09:46

Muhtasari


• Stripchat imeongeza rasmi ofa yetu kwa Everton ili kuwa mshirika rasmi wa kuitwa uwanja mpya wa klabu - Daily Mail.

Hivi karibuni timu ya Everton inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza, EPL ilitangaza mipango yake ya kuhamia uwanja mpya unaoendelea kujenga na ambao utafunguliwa mwanzoni mwa msimu wa 2024/25.

Uwanja huo mpya amabo bado haujapata jina kamili unatarajiwa kusheheni takribani viti elfu 53 vya mashabiki, ambao ni kiwango cha juu kuliko kile amabcho uwanja wao wa sasa wa Goodson Park unasheheni cha mashabiki elfu 40 tu.

Kutokana na uwanja huo mpya bado kutopata jina, makampuni mbali mbali yameanzisha mchakato wa kutuma maombi ili kupata haki za uwanja huo kuitwa jina la kampuni yao.

Jarida la Daily Mail la Uingereza limeripoti habari mpya kabisa kwamba kati ya makampuni ambayo yametuma maombi ya kutaka uwanja huo mpya kupewa jina lao ni kampuni inayojihusisha na mambo ya watu wazima ya StripChat.

Stripchat ni tovuti ya kimataifa ya filamu ya watu wazima na mtandao wa kijamii. Inatoa jukwaa la maonyesho ya kamera ya wavuti yanayotiririshwa moja kwa moja bila malipo, ikijumuisha shughuli za kushiriki mapenzi moja kwa moja kweney kamera.

“Stripchat wamezindua ofa ya pauni milioni 180 wakitaka kupewa haki za kuitwa jina la uwanja wa Everton. Wamekiri kwamba wanatazamia kuuita uwanja mpya wa Everton "Uwanja wa Uendelevu wa Stripchat,” Daily Mail waliripoti.

“Stripchat imeongeza rasmi ofa yetu kwa Everton ili kuwa mshirika rasmi wa kuitwa uwanja mpya wa klabu. Ikiwa ombi letu lingekubaliwa, tungefanya juhudi za makusudi kuufanya 'Stripchat Sustainability Stadium' kuwa wa kimaendeleo zaidi, inayowajibika na endelevu. uwanja wa michezo duniani,” mshirika mkuu wa kampuni hiyo ya mambo ya watu wazima alinukuliwa na Daily Maily.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved