logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Timu ya Barcelona kubadilisha jezi kwa heshima ya rapa Drake

Drake atakuwa akisherehekewa kufikisha mashabiki zaidi ya Bilioni 50 kwenye mtandaoni wa Spotify

image
na Radio Jambo

Habari14 October 2022 - 11:37

Muhtasari


• Jezi hii itakuwa na nembo ya bundi na ambayo itachukua nafasi ya wadhamini wa jezi Spotify kwa ajili ya mchezo muhimu wa kilele dhidi ya Los Blancos.

• Barcelona watakuwa wakilenga kunyakuwa pointi za juu zaidi dhidi ya Real Madrid Jumapili, Oktoba 16.

Rapa Mkanadia Drake

Timu ya soka ya Barcelona ilifichua kuwa itavaa jezi maalum kwa ajili ya mechi ya El Clasico wikendi hii, dhidi ya mahasimu wao Real Madrid katika uwanja wa Santiago Bernabeu Jumapili hii.

Jezi hii itakuwa na nembo ya bundi.

Nembo hii itachukua nafasi ya wadhamini wa jezi Spotify kwa ajili ya mechi hii nzito.

Kubadilishwa kwa jezi hii maalum ni kwa kwa aliji ya Kusherehekewa kwa msanii wa kwanza kuwa na mashabiki zaidi ya Bilioni 50 kwenye nyimbo zake mtandaoni wa Spotify ambaye ni rapa Drake  ambaye asili yake ni Canada.

Rapa Drake anafurahia kushirikishwa kwenye timu ya Barcelona wakati huo.

Majagina hawa wa kabumbu Barcelona, watakuwa na matumaini makubwa ya kuboresha nafasi yao katika jedwali la La Liga. 

Spotify ndio wafadhili wakuu wa jezi za Klabu hii.

Barcelona ikieleza kwenye tuvuti yao ilisema amani yao ni kujiunganisha na mashabiki wengi kote duniani huku wakiahidi kufanya Kolabo na masupastaa mwisho wa muhula huu.

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved