Kiungo wa Chelsea akimbia uwanjani akiwa uchi wa mnyama baada ya sare dhidi ya Man-U

Mkroatia Mateo Kovacic aligeuka gumzo la siku baada ya kuvua nguo zake zote na kuzirisha kwa mashabiki huku akiondoka uwanjani uchi wa mnyama.

Muhtasari

• Baadhi walizua utani kwamba huenda alikuwa anasherehekea sare dhidi ya United, baada ya kuingizwa mchezoni kunako dakika ya 36.

Kiungo huyo wa Chelsea alivua nguo zote akitoka uwanjani
Kiungo huyo wa Chelsea alivua nguo zote akitoka uwanjani
Image: Instagram

Kiungo wa Chelsea Matteo Kovacic alitenga anga na kugeuka gumzo katika uwanja wa Stamford Bridge wakati wa mchezo uliohusisha Manchester United na Chelsea Jumamosi, Oktoba 22 huku akiondoka uwanjani akiwa amevaa nguo zake za ndani tu.

Mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid aliingia uwanjani, akichukua nafasi ya Marc Cucurella dakika ya 36 katika mazingira ya kutatanisha.

Cucurella alitolewa na Graham Potter kwani meneja alionekana kutoridhika na ukweli kwamba alikuwa akicheza nje ya nafasi yake kama benki wa kushoto kila mara.

Chelsea hata hivyo walikuwa timu iliyoboreshwa zaidi baada ya kuingizwa kwa Kovacic, ambaye alionekana kusuluhisha safu ya kiungo ya timu yake. Mashabiki walikuwa wepesi kuashiria athari ya Mcroatia huyo kwenye mchezo lakini mazungumzo yalibadilika haraka hadi kwa mbwembwe zake fupi alipokuwa akiondoka uwanjani.

Video zilizonaswa na kamera na kupakiwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii zilimuonesha kiungo huyo akikimbia kwenye handaki kutoka nje ya uwanja huku akiwa uchi kabisa kando na kubaki na mwanandani yake pekee.

Kwa kawaida, wachezaji huwa wanatoa jezi zao kwa mashabiki baada ya michezo, lakini inaonekana Kovacic, 28, alienda hatua ya ziada. Na hili limetajwa kuwa tukio moja mpya kuwahi kuonekana kwenye ulimwengu wa soka.

Inaarifiwa kuona kama mchezaji huyo atapewa adhabu yoyote ama mamlaka husika zitalifumbia macho tukio hilo la kutoa nguo zote na kuzirisha kwa mashabiki huku akiondoka uwanjani akiwa tupu.

Kwa kawaida, mchezaji anapovua jezi uwanjani huwa analambishwa kandi ya njano, je hili tukio la Kovacic adhabu yake itakuwa gani? Ama litafumbiwa macho kutokana na dhana kwamba lilitokea baada wa kipenga cha mwisho?