Ronaldo, Messi wanaongoza orodha ya wachezaji walioshiriki kombe la dunia 2006

Wachezaji hawa walishiriki kombe la dunia 2006 na mwaka huu nchini Qatar wanatarajiwa kushiriki pia.

Muhtasari

• Hapa tunakuandalia orodha ya baadhi ya wachezaji ambao walishiriki mashindano ya kombe la dunia 2006 na ambao wanatarajiwa kushiriki mashindano hayo mwaka huu.

Wachezaji walioshiriki kombe la dunia 2006 na ambao watashiriki 2022 Qatar
Wachezaji walioshiriki kombe la dunia 2006 na ambao watashiriki 2022 Qatar
Image: Instagram

Muda unazidi kwenda, na wiki sasa zinazidi kupukutika kuwa siku. Takribani siku 18 tu ndio zimesalia kuelekea mashindano makubwa zaidi katika malimwengu ya soka – Kombe la dunia!

Mnamo Novemba 20, kampeni za mashindano hayo zitang’oa nanga rasmi nchini Qatar na jumla ya mataifa 32 yatashiriki katika kipute hicho kinachofuatiliwa pakubwa kote ulimwenguni.

Lakini je, unafahamu kwamba katika mashindano ya kombe la dunia yaliyofanyika mwaka 2006 nchini Ujerumani, mpaka sasa ni wachezaji wachache sana ambao bado wanaendeleza taaluma zao za kandanda?

Hapa tunakuandalia orodha ya baadhi ya wachezaji ambao walishiriki mashindano ya kombe la dunia 2006 na ambao wanatarajiwa kushiriki mashindano hayo mwaka huu nchini Qatar, miaka 16 baadae!

Lionel Messi

Argentina walikuwa washindani wa kuogopwa wa Kombe la Dunia la 2006, na kuwa vivutio vya wasioegemea upande wowote kwa kandanda ya mashambulizi ya kudumu na kwa ujumla inaonekana kama wanacheza mchezo tofauti na Uingereza.

Messi kipindi hicho akiwa mwenye umri wa miaka 18 alifunga wakati wa mchezo wa 6-0 dhidi ya Serbia na Montenegro na kusababisha bao lililokataliwa kuwa la kuotea wakati wa ushindi wa hatua ya 16 bora dhidi ya Mexico.

Kwa bahati nzuri, Messi ametumia muda wake wote wa maisha kuthibitisha kuwa yeye ni mmoja wa wanasoka bora zaidi kuwahi kucheza mchezo huo - hata PSG mwaka huu.

Mchezaji huyo amabye sasa ana miaka 33 anatarajiwa kuiongoza timu ya taifa ya Argentina katika kusaka ubingwa nchini Qatar.

Cristiano Ronaldo

Mashindano ya Ronaldo ya 2006 yalikuwa yanahusu ‘kukonyeza macho’. Alikuwa mmoja wa wachezaji bora katika Kombe la Dunia wakati Ureno ilifika nusu fainali.

Fowadi huyo wa Manchester United alifunga bao lake la kwanza kwenye Copa Mundial - penalti dhidi ya Iran katika hatua ya makundi - na kwa ujumla alimshinda Luis Figo wakati nchi yake ikifurahia Kombe lao bora la Dunia tangu 1966.

 

Kwa zaidi ya miaka kumi tangu hapo Ronaldo ameibukia kuwa mfungaji bora wa Ureno - na wa kimataifa wa kandanda - na amewafanya wengi katika kizazi chake pamoja na Messi kuupenda mchezo wa kandanda.

Kando na wingi wa tuzo za klabu, Ronaldo pia ameiongoza Ureno kutwaa Ubingwa wa Ulaya na mataji ya UEFA Nations League. Akiwa na umri wa miaka 37, atatafuta kunyanyua Kombe la Dunia huko Qatar.

Luka Modric

Modric alikuwa chipukizi mwenye sura mpya miaka 16 iliyopita, akifanya mechi mbili akitokea benchi huku Croatia ikitoka nje katika raundi ya kwanza.

Kiungo huyo alitunukiwa Mpira wa Dhahabu mwaka wa 2018 huku Croatia wakiwashangaza wengi kwa kutinga fainali na atakuwa msingi wa matumaini yao ya kucheza mechi hizo za Qatar.

Kando na hayo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 anasalia kuwa muhimu kwa kikosi cha Real Madrid na alifurahia mchezo mzuri wakati wa ushindi wao wa hivi majuzi dhidi ya Bercelona.

Zlatan Ibrahimovic

Kombe la Dunia la 2022 huenda likawa ndio la mwisho kwa staa huyo wa AC Milan kushiriki kutokana na umri kumuacha.

Licha ya kuumbwa na majeraha kwa mrundiko, mchezaji huyo bado anatarajia kuiwakilisha timu yake ya Uswidi katika mashindano ya kombe la dunia mwaka huu nchini Qatar.

Mwaka wa 2006, Ibrahimovic alikuwa na miaka 24 pekee na baada ya Uswidi kuondolewa katika kipute hicho katika awamu ya 16 bora, alihama kutoka Juventus kwenda Inter Milan msimu huo wa joto na ametumia muda wake wote wa kazi akipachika mabao na sifa katika baadhi ya vilabu bora Ulaya.

Sergio Ramos

Beki matata wa Uhispania ambaye kwa muda mrefu amekuwa akichezea timu ya Real Madrid kabla ya kujiunga na PSG msimu jana.

Sergio Ramos alifunga mara mbili wakati wa ushindi wa 6-0 dhidi ya San Marino katika mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la FIFA la 2006. Uchezaji wake, kwa Uhispania na Real Madrid, ulimhakikishia nafasi kwenye kikosi cha Kombe la Dunia mwaka huo.

Mwaka huu japo amekuwa akikumbwa na majeraha, lakini kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uhispania, Luiz Enrique amearifiwa kumjumuisha katika kikosi cha watu 55 kitakachoshiriki mchujo wa kupunguza hadi wachezaji 26 watakaosafiri kuenda Qatar wiki mbili zijazo.