Kombe la Dunia 2022: Sadio Mane kushikiriki licha ya kuwa na majeraha

Mshambulizi huyo alilazimika kutoka nje katika mechi ya Bayern Munich dhidi ya Werder Bremen.

Muhtasari

• Senegal itaanza mashindano ya Kundi A dhidi ya Uholanzi tarehe 21 Novemba.

Image: BBC

Sadio Mane amejumuishwa kwenye kikosi cha Senegal kitakachoshiriki Kombe la Dunia nchini Qatar licha ya kusumbuliwa na majeraha siku ya Jumanne.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30 alilazimika kutoka nje katika kipindi cha kwanza cha ushindi wa 6-1 wa Bayern Munich dhidi ya Werder Bremen.

Mabingwa hao wa Ujerumani walisema alipata jeraha "katika eneo la goti" na ataukosa mchezo wa Jumamosi dhidi ya Schalke.

Senegal itaanza mashindano ya Kundi A dhidi ya Uholanzi tarehe 21 Novemba.

"Tunafuatilia hali ilivyo na tumemtuma mmoja wa madaktari wetu kumpima," kocha wa Senegal Alioy Cisse alisema katika mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu wa Senegal Dakar siku ya Ijumaa.

"Siku ya Alhamisi, Sadio alikaa siku nzima mjini Munich kabla ya kusafiri kwenda Austria kwa vipimo zaidi. Habari njema ni kwamba hahitaji kufanyiwa upasuaji. "Tunataka hali kubadilika katika wiki mbili-tatu. Sitaki kumtenga."

Akiwa mfungaji bora wa mabao nchini mwake, akiwa na mabao 34 katika mechi 93, utimamu wa Mane ndio ufunguo wa nafasi za Senegal na Cisse atatoa jasho kwa upatikanaji wake kabla ya mechi yao ya kwanza dhidi ya Uholanzi, mechi dhidi ya wenyeji Qatar (Novemba 25) na Ecuador (Novemba 29).