Fenerbahce wamuongeza Valencia kwenye picha ya mastaa Ronaldo na Messi

Kitendo hicho kinakuja siku moja tu baada ya mchezaji huyo kutinga mabao mawili na kuisaidia Ecuador kuilemea Qatar katika mechi ya ufunguzi kombe la dunia.

Muhtasari

• Ronaldo na Messi kwa mara ya kwanza walionekana kweney picha ya pamoja nje ya uwanja, picha ambayo imezungumziwa sana duniani.

Messi na Ronaldo katika picha ambayo Valencia aliongewa kupitia photoshop
Messi na Ronaldo katika picha ambayo Valencia aliongewa kupitia photoshop
Image: Twitter

Jumapili mashindano ya kombe la duni yaling’oa nanga nchini Qatar ambapo wenyeji walifungua uwanja dhidi ya Ecuador majira ya saa moja jioni.

Katika mechi hiyo ambayo iliona rekodi ya miaka 92 kuvunjiliwa mbali, Ecuador walikiuka adabu za mgeni na kumchachafya mwenyeji mabao mawili kwa nunge mbele ya umati wa mashabiki wa nyumbani.

Mabao yote mawili yalifungwa na aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Manchester United ambaye sasa anaitumiakia Fenerbahce ya Uturuki, Enner Valencia.

Kufuatia kufungwa kwao mechi ya ufunguzi, Qatar iliingia kweney vitabu vya historia kuwahi kuwa taifa la kwanza kupoteza mechi ya ufunguzi nyumbani katika mashindano ya kombe la dunia, rekodi ambayo ilikuwa imedumu kwa miaka 92.

Valencia alifana katika mechi hiyo na aliibuka kuwa mchezaji bora na kutuzwa. Klabu yake ya Fenerbahce ilifurahia weledi wake na hawakusita kuihariri picha yake kando na picha ya masupastaa wawili wa soka Christiano Ronaldo na Lionel Messi – picha ambayo ilipakiwa katika mitandao ya kijamii ya mastaa hao Jumamosi usiku.

Wengi walisema kuwa picha hiyo ya Ronaldo na Messi ni moja ya picha ambazo zitaenda chini kama picha ya karene kwani haijawahi tokea waonekanai wakiwa pamoja nje ya uwanja wakipunga upepo kwa kufurahia mchezo wa chess.

Kitendo cha Fenerbahce kupakia picha hiyo ambayo walikuwa wameifanyia uhariri wa kiwango cha juu kwa kimombo Photoshop, walinuia kutuma ujumbe kuwa Valencia amejinafasi kando na wachezaji wawili mastaa wakubwa na kuwa yeye ndiye staa wa tatu baada ya kung’ara katika mechi ya ufunguzi wa kombe la dunia.