Aliyebashiri Argentina kuishinda Saudia apoteza Ksh 19.5M kwa kamari

Alipoteza beti hiyo baada ya Saudi Arabia kuwacharaza Argentina mabao 2-1.

Muhtasari

• Jamaa huyo angeshinda  milioni 22.1 ikiwa ni faida ya milioni 2.1 ya kile alichokuwa amewekeza.

Image: Maktaba

Huku timu ya Saundi  Arabia ikirukaruka na kusherehekea kwa kuwatandika Argentina, jamaa mmoja analia kwikwikwi baada yake kupoteza beti aliyokuwa ameibashiria timu ya Argentina ili kuibuka washindi.

Jamaa huyo raia wa Australia alihuzunika sana baada ya kupoteza kima cha shilingi Milioni 19.5 aliyokuwa amebashili, beri ambayo ingempa Milioni 22.1, ikiwa ni faida ya milioni 2.1 za pesa alizokuwa amebashiria mwanzo.

Mashabiki wa Argentina walisikika kwenye uwanja wakipiga vifijo na nderemo baada Lionel Messi kufunga bao la kwanza dakika ya 10 kupitia mkwaju wa penalti kwenye kipindi cha kwanza.

Lakini kinyume na matarajio, Argentina wakapokea pigo la mwaka baada ya mchezaji wa Saudia kufunga bao la kusawazisha na kufutilia bao la Lionel Messi.

Bao la mchezaji Salem Al-Dawsari wa Saudia alilolifunga dakika nne baaada ya kurejea kutoka mapumzikoni lilibadilisha taswira ya uwanja huo huku wapenzi wa soka wakikosa kuamini jinsi timu kama hiyo maarufu ilivyoshindwa.

Saudi Arabia iliwashinda mahasimu wao Argentina mabao 2-1 huku historia ikiwekwa kutokana na ushindi huo.

Duru za kuaminika zinaripoti kuwa mcheza kamari mwingine aliwekeza milioni 12.2 kwa Argentina kushinda kwa zaidi ya mabao  5 dhidi ya Saudi Arabia, pia alienda nyumbani bila chochote.