Raia wa Saudia avunja mlango baada ya timu yao kushinda Argentina 2-1 (video)

Mwanamume huyo aliuvunja mlango wake baada ya bao la pili la Saudi Arabia kuhakikisha ushindi.

Muhtasari

• Saudi Arabia waliwafunga Argentina mabao mawili ndani ya dakika 4 pekee katika kipindi cha pili na kulifutilia mbali bao la Lionel Messi  alilolifunga kupitia mkwaju wa penlati.

• Angentina kufungwa ni jambo la ajabu na la kihistoria lililowahi kutokea katika malimwengu ya soka.

Shabiki wa kambumbu wa Saudi Arabia mwenye furaha isiyopimika aliuvunja mlango wa nyumba aliposherehekea bao la ushindi katika ushindi wao wa kushangaza wa 2-1 dhidi ya Argentina.

Wachezaji wa Saudi Arabia walishangaza ulimwengu kwa jumla  baada ya kufunga mabao mawili ndani ya dakika 4 pekee katika kipindi cha pili. Tukio hilo la Angentina kufungwa ni jambo la ajabu na la kihistoria lililowahi kutokea katika dunia ya wanasoka. Pia lililetea sononeko sio tu kikosi kizima cha timu hiyo bali pia mashabiki.

Lionel Messi alianza kufunga kwa mkwaju wa penalti dakika ya 10 ya mechi, lakini bao lake lilikatizwa na mabao ya Saleh Al-Shehri na Salem Al-Dawsari.

Bao lake la pili Al-Dawsari,  liliwafanya mashabiki wa Saudia kusherehekea kwa fujo huku shabiki mmoja aking'oa mlango kutoka kwa bawaba za mlango na kwenda kuitumpa inje.

Mashabiki wa soka wamejitokeza kwenye mitandao ya kijamii kuonyesha kufurahishwa na msisimko ulioonyeshwa na shabiki shakiki huyo wa Saudia.

Mmoja alisema: 'Kandanda pekee ndiyo inaweza kukufanya uhisi hivi''

Wa pili aliandika: 'Kombe la Dunia halijashindwa bado kuna matumaini kwa timu ya Argentina.''

Video hiyo ilipata zaidi ya watazamaji Milioni 1.

Mashabiki wa Saudi Arabia pia walirekodiwa wakiwakejeli Lionel Messi na Argentina.