logo

NOW ON AIR

Listen in Live

(Video) Ronaldo achomoa kitu kutoka sehemu nyeti na kutia mdomoni mechi ikiendelea

Tukio hili lilitokea wakati Ureno walikutana na Ghana katika mechi yao ya kwanza kwenye kundi H.

image
na Radio Jambo

Makala25 November 2022 - 12:52

Muhtasari


• Mechi hiyo iliisha kwa faida ya Ureno ambao waliwazamisha Ghana kwa kibano cha mabao 3-2.

Alhamisi usiku timu ya taifa ya Ureno ilicheza mechi yake ya kwanza katika mashindano ya kombe la duni ya mwaka huu nchini Qatar dhidi ya Nyota Weusi, timu ya taifa ya Ghana.

Mechi ambayo iliweka historia katika mashindano hayo kwani Ghaja japo walilemewa kwa mabao matatu kwa mawili, walikuwa timu ya kwanza kabisa kutoka Afrika kufunga bao katika mashindano hayo nchini Qatar.

Katika mechi hiyo ambayo ilikumbwa na utata mwingi kutoka kwa refa hasa baada ya kuwatunuku Ureno penalty yenye utata iliyotiwa wavuni na staa Ronaldo, mchezaji huyo alionekana akifanya kitendo ambacho kimeibua gumzo kali mitandaoni.

Katika video moja ambayo imekuwa ikisambazwa mitandaoni, Ronaldo alionekana akitoa kitu fulani ndani ya kaptula yake upande wa mbele katika sehemu yake nyeti na kukitia mdomoni kabla ya kuanza kukitafuta huku akikimbia.

Kitendo hicho kimeibua mjadala mkali huku kila mtu akionekana kuachwa kinywa wazi kwani mpaka sasa hakuna anayejua Ronaldo ni kitu kipi kile alikitoa katika tupu yake ya mbele na kutia mdomoni, na hata yeye mwenyewe hajazungumzia video hiyo.

Katika mechi hiyo, Ghana walijitahidi kwa udi na ambary kutafuta ushindi huku Ureno nao wakicheza vizuri hadi kipindi cha kwanza kikakamilika bila timu yoyote kuona lango la mwingine.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo Ureno walipata penalty yenye utata baada ya benki kumuangusha Ronaldo aliyeinuka na kutia penalty kinywani. Wachezaji wenza Joao Felix na Rafael Leao walifunga mabao mengine mawili na Ghana kufunga yao mawili kupitia wachezaji Andre Ayew na Osman Bukari ambaye aliiga kusherehekea maarufu kwa Ronaldo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved