Wanyama na Mariga wanafaa kuongoza soka Kenya - Winnie Odinga

Alisema kuwa hao ndio watakuwa tiba katika soka yetu kwani nchini Cameroon aliyekuwa staa wao, Etoo tayari amenyoosha mambo kisoka.

Muhtasari

• Kulingana na Winnie, Kenya inafaa kuwapa kipaumbele wachezaji wa zamani kama McDonald Mariga na nduguye Victor Wanyama kuchukua usukani.

Winnie apendekeza Wanyama na Mariga kuongoza soka Kenya
Winnie apendekeza Wanyama na Mariga kuongoza soka Kenya
Image: instagram

Binti wa kigogo wa kisiasa nchini Kenya Raila Odinga, Winnie Odinga ametoa wazo lake kuhusu jinsi Kenya inaweza pata tiba katika masuala ya uongozi wa michezo haswa kandanda nchini Kenya.

Winnie ambaye ni mmoja wa Mbunge wa Kenya aliyechaguliwa hivi karibuni katika Bunge la Afrika Mashariki alikuwa na maoni kwamba vyombo vya soka vya Kenya vinapaswa kuongozwa na wanasoka wa kitaalamu na sio vinginevyo.

Aliandika maoni haya kupitiqa ukurasa wake wa Twitter na kutolea mfano kuwa suluhu kama hilo tayari limeonekana kuzaa matunda upande wa Cameroon ambapo aliyekuwa staa wao Samuel Etoo ndiye sasa anaongosha shirikisho la soka nchini humo.

 “Kuona Samuel Eto’o akitazama nchi yake ikicheza Kombe la Dunia kama Rais wa Shirikisho la Soka kunanifanya niamini zaidi kwamba wachezaji wetu wa zamani wanapaswa kuongoza vyombo vyetu vya Soka,” Winnie Oding akliandika.

Kulingana na Winnie, Kenya inafaa kuwapa kipaumbele wachezaji wa zamani kama McDonald Mariga na nduguye Victor Wanyama kuchukua usukani katika kunyoosha sekta ya kandanda angalau nasi tuone Harambee Stars wakati mmoja ikipeperusha bendera ya kitaifa katika ulingo wa kimataifa kama AFCON na FIFA  kombe la dunia.

“Mariga anafaa kuja kuhamisha ujuzi ambao yeye na Victor (Wanyama) walijifunza kutoka kwa Noah (Wanyama, mwanasoka mashuhuri, mchezaji wa zamani wa Harambee Stars na kocha wa zamani wa AFC Leopards. Yeye pia ni baba wa ndugu hao)," Winnie Odinga alisema.

Ndugu hao- Mariga na Wanyama- wana taaluma kubwa katika soka tangu mwanzo duni nchini Kenya hadi kucheza katika mechi za kimataifa kwa vilabu mbalimbali.

Mariga alianzia Tusker FC, Ulinzi Stars, Kenya Pipeline na Harambee Stars kabla ya kwenda kuchezea timu za kigeni zikiwemo Inter Milan, Enköpings SK, Helsingborgs IF, Parma, Internazionale, Real Sociedad, Latina, Real Oviedo na Cuneo Calcio.

Kwa upande mwingine Wanyama alichezea Nairobi City Stars, AFC Leopards, Helsingborg, Beerschot, Celtic, Southampton, Tottenham Hotspur, na CF Montréal, ambako anacheza kwa sasa.