Kombe la Dunia 2022: Cristiano Ronaldo 'mwenye fikra kamili za kiakili’ kwa kushinda penati ya Ureno – Fifa

mjumbe wa Kikundi cha Fifa cha kiufundi(TSG) , Sunday Oliseh alisema washambuliaji "wanakuwa bora zaidi".

Muhtasari
  • TSG, ambayo inaongozwa na meneja wa zamani wa Arsenal manager Arsene Wenger, hutazama kila mechi na kutoa tathmini
Image: INSTAGRAM// CHRISTIANO RONALDO

Cristiano Ronaldo ameitwa "mwenye fikra kamli za kiakili’ kamili na Fifa kwa jinsi alivyoshinda bao la penati ya Ureno katika ushindi wao katika mechi Kombe la Dunia dhidi ya Ghana.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 37 alikuwa mtu wa kwanza kufunga magoli ya penati katika mashindano Matano tofauti ya Kombe la Dunia, baada ya kufunga bao kwa mkwaju wa penati.

Ureno ilishinda 3-2, lakini kutolewa kwa penati kulimghadhabisha menja wa Ghana Otto Addo, ambaye alisema "haikuwa penati ".

Katika mkutano wa wandishi wa habari mjini Doha, mjumbe wa Kikundi cha Fifa cha kiufundi(TSG) , Sunday Oliseh alisema washambuliaji "wanakuwa bora zaidi".

TSG, ambayo inaongozwa na meneja wa zamani wa Arsenal manager Arsene Wenger, hutazama kila mechi na kutoa tathmini ikiwa ni pamoja na data za ubora wa uchezaji na mitindo ya mchezo.