logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Baada ya Ghana kuipiga Korea, kocha wao achukua selfie na Son Heung-Min akilia (+video)

Korea Kusini ilipoteza 2-3 kwa vijana wa Otto Addo katika mchuano wao wa pili wa Kombe la Dunia

image
na Radio Jambo

Makala29 November 2022 - 04:56

Muhtasari


•Son Heung-Min aliachwa akiwa na huzuni kubwa baada ya  Korea Kusini kupoteza mechi hiyo iliyojaa wasiwasi.

•Kocha wa Korea Paul Bento alionyesha kadi nyekundu baada ya mchuano huo kwa kuharakisha kumtusi refa Anthony Taylor.

Jumatatu jioni haikuwa nzuri kwa timu ya soka ya Korea Kusini baada ya kulambishwa sakafu na timu ya Ghana katika mechi yao wa Kombe la Dunia.

Korea Kusini ambayo inaongozwa na mkufunzi Paulo Bento ilipoteza 2-3 kwa vijana wa Otto Addo katika mchuano wao wa pili wa Kombe la Dunia na kudidimiza matumaini yao ya kuhitimu kusonga mbele kuingia hatua ifuatayo ya mashindano hayo.

Mshambulizi wa Tottenham Hotspur Son Heung-Min aliachwa akiwa na huzuni kubwa baada ya  Korea Kusini kupoteza mechi hiyo iliyojaa wasiwasi. Mshambulizi huyo wa matata alishindwa kabisa kujizuia wakati akijaribu kukubaliana na matokeo hayo huku wachezaji wenzake, wakufunzi na wapinzani wakijaribu kumfariji.

Mmoja wa wakufunzi wa Ghana hata hivyo alionekana akijaribu kupiga picha ya selfie na mchezaji huyo huku wakufunzi wenzake wawili wakijaribu kumtia moyo. Baada ya tukio hilo Son alisonga kando na kujishika magoti  kwa huzuni.

Kocha wa Korea Paul Bento alionyesha kadi nyekundu baada ya kuzozana na marefa juu ya kumaliza mchezo mapema.

Ingawa Korea Kusini ilikuwa nyuma katika dakika za mwisho, matumaini yote hayakuwa yamepotea kwani dakika 10 ziliongezwa mwishoni mwa kipindi cha pili.  Korea ilitengeneza nafasi nzuri zaidi baada ya kwenda nyuma, ilipata kona katika hatua ya mwisho ya muda wa nyongeza wa kipindi cha pili.

Timu hiyo iliamini wangepata nafasi ya mwisho ya kusawazisha lakini Taylor alipuliza kipenga cha kumaliza mchezo baada ya mpira kutoka nje na kuwa kona, na kuibua hasira miongoni mwa wachezaji na wakufunzi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved