Kolo Toure ateuliwa kuwa kocha wa Wigan Athletic

Muhtasari

• Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 41 anachukua nafasi ya Leam Richardson baada ya kutimuliwa na klabu hiyo mapema mwezi huu.

Beki wa zamani wa Ivory Coast, Arsenal na Manchester City Kolo Toure.
Beki wa zamani wa Ivory Coast, Arsenal na Manchester City Kolo Toure.
Image: Getty Images

Wigan Athletic imemteua beki wa zamani wa Ivory Coast, Arsenal na Manchester City Kolo Toure kuwa meneja wao mpya kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 41 anachukua nafasi ya Leam Richardson baada ya kutimuliwa na klabu hiyo mapema mwezi huu.

Raia huyo wa Ivory Coast ametumia miaka mitano iliyopita kufundisha Celtic na Leicester City chini ya Brendan Rodgers lakini hili ni jukumu lake la kwanza katika usimamizi.

Mchezo wa kwanza utakaosimamiwa na Toure utakuwa safari ya kuelekea Millwall tarehe 10 Desemba.

Wigan wako katika nafasi ya 22 kwenye jedwali, lakini walishinda mchezo wao wa mwisho dhidi ya Blackpool kabla ya mapumziko ya Kombe la Dunia.

"Tuna furaha kwamba Kolo amekuwa meneja mpya wa Klabu ya Soka ya Wigan Athletic, na bodi ina imani kwamba yeye ndiye mtu atakayetupeleka mbele," mtendaji mkuu Malachy Brannigan aliambia tovuti ya klabu.