logo

NOW ON AIR

Listen in Live

KFC washambuliwa kwa kumlinganisha Ronaldo na Aboubakar wa Cameroon

Ronaldo amekuwa akihusishwa na kujiunga Al-Nassr, timu Aboubakar anaitumikia.

image
na Davis Ojiambo

Michezo06 December 2022 - 09:39

Muhtasari


  • • “Chaguo bora la akiba kwa Aboubakar kusema kweli,” KFC waliandika.

Mkahawa wa maduka ya vyakula vya haraka KFC umeibua mgawanyiko mkubwa mitandaoni baada ya kuibua madai ambayo yalilenga kumdunisha staa namba moja wa kandanda duniani, Mreno Christiano Ronaldo.

Kupitia Tweet ambayo KFC walinukuu, wengi walihisi kuwa wanamdunisha Ronaldo waliposea kuwa mchezaji huyo ambaye sasa hana klabu baada ya mkataba wake na Manchester United kusitishwa, kuwa anaweza akawa mshambuliaji wa akiba nyuma ya mshambuliaji wa Cameroon Aboubakar.

KFC walinukuu tweet ya blogu moja kwa jina Madrid Zone kwenye Twitter ambao walitoa taarifa kwamba Ronaldo ameafikiana mkataba wa miaka miwili na nusu na klabu moja nchini Saudi Arabia, ambapo duka hilo la vyakula vya haraka lilisema ni chaguo bora la akiba kama mshambuliaji mbadala wa Aboubakar.

“Christiano Ronaldo ataitumikia Al-Nassr kutoka Januari mosi kwa mkataba wa miaka miwili unusu kwa dau la pauni milioni 200 kwa msimu mmoja. Dili limekamilika,” Madrid Zone walisema.

“Chaguo bora la akiba kwa Aboubakar kusema kweli,” KFC waliandika.

Mkataba wake ulikatishwa baada ya kufanya mahojiano ya uhakika na Piers Morgan ambapo alilipuka vikali kuhusu klabu hiyo. Kwa sasa anaangazia kampeni ya Ureno ya Kombe la Dunia lakini Januari, atalazimika kupata klabu mpya kutokana na kwamba ameeleza nia yake ya kuendelea kucheza hadi atakapofikisha miaka 40.

Aboubakar ndiye mshambuliaji wa kutegemewa wa klabu ya Al-Nassr. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 alifunga bao moja, ambalo ni la kukumbukwa zaidi dhidi ya Brazil. Uwezo wake wa kupachika mabao hauzungumzwi lakini kumlinganisha na Ronaldo kunaweza kuwa mkubwa.

Ronaldo mara nyingi anachukuliwa kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi duniani pamoja na Lionel Messi. Kuhamia kwake Mashariki ya Kati bila shaka kutakuwa na athari kubwa licha ya viwango vyake vya uchezaji kudorora hivi karibuni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved