logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Eto'o aomba radhi baada ya ugomvi na shabiki wa Algeria

Eto'o alikashifu uchokozi na unyanyasaji wa kila siku wa baadhi ya wafuasi wa Algeria.

image
na Davis Ojiambo

Michezo07 December 2022 - 07:58

Muhtasari


  • • "Baada ya mechi ya Brazil na Korea Kusini, nilikuwa na ugomvi mkali na mtu ambaye pengine alikuwa mfuasi wa Algeria," Eto'o alisema.

Rais wa shirikisho la soka nchini Cameroon Samuel Eto'o amejitokeza na kuomba radhi kwa kuhusiana na ugomvi na mwanamume mmoja nje ya uwanja wa Kombe la Dunia nchini Qatar.

Katika taarifa yake, Eto'o alikashifu uchokozi usiokoma na unyanyasaji wa kila siku wa baadhi ya wafuasi wa Algeria.

"Baada ya mechi ya Brazil na Korea Kusini, nilikuwa na ugomvi mkali na mtu ambaye pengine alikuwa mfuasi wa Algeria," Eto'o alisema.

"Ningependa kuomba radhi kwa kushindwa kujizuia na kujibu kwa njia ambayo hailingani na utu wangu. Naomba radhi kwa umma kwa tukio hili la kusikitisha."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved