Messi awadhalilisha mabeki 3 wa Uholanzi kwa chenga za kimaudhi kabla ya kutoa pasi ya bao

Katika picha hiyo, Messi anaonekana akiwageuza pande zote mabeki wakiongozwa na Van Dijk na kuwaacha nyuma kwa kasi za ajabu.

Muhtasari

• Argentina waliwalemea Uholanzi kupitia mikwaju ya penalti na watakutana na Croatia kwenye nusu fainali.

• Croatia waliwaondoa Brazil pia katika matuta ya penalti.

Messi akiwaacha hoi bin taaban mabeki wa Uholanzi.
Messi akiwaacha hoi bin taaban mabeki wa Uholanzi.
Image: Twitter

Nahodha wa Argentina Lionel Messi kwa mara nyingine alidhihirisha uchawi wake uwanjani taifa lake walipokuwa wanagaragazana na Uholanzi katika mechi ya kufuzu nusu fainali kombe la dunia inayoendelea Qatar.

Katika picha ambazo zimekuwa zikisambazwa mitandaoni, Messi aliwageuza mazamwamwa mabeki wa Uholanzi watatu kabla ya kuwaacha nyuma na kukimbia mbele na mpira kwa kasi za duma na kumpakulia pasi nyerezi mwenzake Nahuel Molina aliyezamisha mpira wavuni na kuwapa Argentina uongozi wa mechi hiyo hiyo kunako kipindi cha kwanza.

Na kisha, katika dakika ya 73, Messi alidhihirisha uwepo wake alipojipanga kupiga mkwaju wa penalti. Huku mkwaju wa kasi ukiwa chini na kulia, Messi alimbwaga kipa na kuendeleza uongozi wa Argentina hadi 2-0.

Licha ya kuwa chini kwa mabao 2-0, Waholanzi hawakukata tamaa. Dakika ya 83, Wout Weghorst aliyetokea benchi aliichambua safu ya ulinzi ya Argentina na kutoboa lango na kuifanya Uholanzi kupinguza ushinde kwa mabao 2-1.

Ndani ya dakika za lala salama (90'+11), Weghorst alifunga tena kwa seti nzuri iliyosawazisha matokeo 2-2 kabla ya mwamuzi kumalizia kanuni na kulazimisha dakika 30 za muda wa ziada. Bado haikutosha kuamua mshindi.

Mchezo huo ulienda kwa mikwaju ya penalti ambapo kipa wa Argentina Emiliano Martinez aliduwaa - kuzuia majaribio mawili ya kwanza ya Uholanzi - huku Argentina ikifunga katika majaribio yao matatu ya kwanza kushinda 2-2 (4-3).