Rais wa Marekani, Joe Biden ailiwaza Morocco baada ya kubanduliwa na Ufaransa

Biden alikuwa amekongamana na marais wa Afrika katika mkutano wa siku tatu Washington DC.

Muhtasari

• Biden alisema kuwa timu hiyo ilifana sana katika mashindano hayo na kuwashangaza wengi.

Rais wa Marekani akiwa na viongiz wa Afrika kutazama mechi
Rais wa Marekani akiwa na viongiz wa Afrika kutazama mechi
Image: Twitter

Rais wa Marekani Joe Biden ametuma ujumbe wa kuwaliwaza Morocco baada ya kushindwa kufuzu fainali ya kombe la dunia huko Qatar usiku wa kuamkia Ijumaa.

Morocco ilikuwa timu ya kwanza kutoka bara la Afrika kutinga nusu fainali na wengi walikuwa wamejitupa nyuma yao katika mecho ya nusu fainali dhidi ya Ufaransa – mecho ambayo iwapo wangrshinda basi wamekuwa taifa la kwanza la Afrika kushiriki fainali za kombe la dunia ambapo itafanyika Jumapili wikendi hii.

Morocco waliibuka washindwa kwa kufungwa mabao mawili kappa na Ufaransa ambayo sasa itakutana na Argentina kwenye kipute cha fainali kupata bingwa wa dunia katika soka.

Rais Biden ambaye alikuwa amekongamana na marais kutoka bara la Afrika nchini humo kupitia ukurasa wake wa Twitter aliiandikia Morocco ujumbe wa kuwatia moyo huku akiwasifia kwa hatua ya kufika nusu fainali.

“Ilikuwa heshima kubwa kutazama mechi ya leo ya Kombe la Dunia pamoja na Waziri Mkuu Akhannouch wa Morocco. Haijalishi unampigia upato nani, ilipendeza sana kutazama ni kiasi gani timu hii imeweza kufikia,” Biden alisema.

Viongozi wa Afrika walikusanyika Washington D.C wiki hii kuhudhuria Mkutano wa siku tatu wa Viongozi wa USA na Africa. Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2014, Umoja wa Afrika, wakiwemo viongozi 45 wa mataifa ya Afrika, na wajumbe kutoka nchi 49 wanashiriki katika hafla hiyo ya siku tatu.

Rais huyo wa awamu ya 46 amekuwa akionekana kuzungumzia sana masuala ya kandanda haswa tangu mashindano ya kombe la dunia yang’oe naga mwezi jana huko Qatar.

Timu ya taifa la Marekani iliondolewa katika hatua ya 16 bora ilipochabangwa na Uholanzi.