Fainali ya Kombe la Dunia: Messi 'anataka kuendelea' kuichezea Argentina

Messi atafikisha miaka 36 mwaka ujao lakini anaamini ana mengi ya kuipatia taifa lake.

Muhtasari

•Lionel Messi anasema hatastaafu soka la kimataifa baada ya kuiongoza Argentina kunyakua kombe la dunia.

•"Aliongeza: "Ni wazi nilitaka kumaliza kazi yangu na hii na siwezi kuuliza chochote zaidi.

Lionel Messi
Image: BBC

Lionel Messi anasema hatastaafu soka la kimataifa baada ya kuiongoza Argentina kunyakua kombe la dunia kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 36.

Mshambulizi huyo wa Paris St-Germain aliulizwa kuhusu mustakabali wake na kituo cha televisheni cha Argentina TyC Sports baada ya ya taifa hilo la Amerika Kusini kuilaza Ufaransa kwa mikwaju ya penalti 4-2 kufuatia sare ya 3-3.Messi atafikisha miaka 36 mwaka ujao lakini anaamini ana mengi ya kuipatia taifa lake.

"Ninapenda soka, ndivyo ninavyofanya," alisema.

"Ninafurahia kuwa katika timu ya taifa na ninataka kuendelea kwa kushuhudia michezo michache zaidi kama bingwa wa dunia.

"Aliongeza: "Ni wazi nilitaka kumaliza kazi yangu na hii na siwezi kuuliza chochote zaidi.

"Messi, akicheza Kombe lake la tano la Dunia, alifunga mara mbili kwenye fainali na pia alifunga penalti kwenye mikwaju ya penalti.Alishinda Mpira wa Dhahabu wa mashindano hayo - uliotunukiwa mchezaji bora - baada ya kufunga mabao saba.

Messi atakuwa na umri wa miaka 39 wakati wa Kombe lijalo la Dunia na alikuwa amedokeza hapo awali kwamba toleo hili nchini Qatar lingekuwa la mwisho kwake.

Hata hivyo, kocha Lionel Scaloni anasema anamtaka Messi katika kikosi chake kwa ajili ya michuano ya 2026, itakayofanyika Marekani, Canada na Mexico.

"Kwanza kabisa, tunahitaji kumwekea nafasi katika kikosi chate cha Kombe lijalo la Dunia 2026," alisema."Ikiwa anataka kuendelea kucheza, atakuwa nasi.

Nafikiri ana haki zaidi ya kuamua kama anataka kuendelea kuichezea Argentina au la, au anachotaka kufanya katika maisha yake ya soka."Ni furaha kubwa kwetu kumfundisha yeye na wachezaji wenzake.

"Kila kitu anachokutana nacho hadi wachezaji wenzake ni kitu kisicho na kifani, kitu ambacho sijawahi kuona. Mchezaji, mtu anayetoa sana kwa wenzake."