Tutarudi- Mbappe hatimaye azungumza baada ya Ufaransa kushindwa katika kombe la dunia

Mshambuliaji wa Ufranasa ataondoka Qatar kama mfungaji bora zaidi wa shindano

Muhtasari
  • Timu ya Mbappe ilishika nafasi ya pili baada ya Argentina kuifunga Ufaransa 4-2 kwa mikwaju ya penalti
Mbappe akanusha kutaka kuondoka PSG
Mbappe akanusha kutaka kuondoka PSG
Image: Maktaba

Kylian Mbappe ametangaza kwamba watarejea kwa ukubwa na bora zaidi katika Kombe la Dunia la 2026.

Timu ya Mbappe ilishika nafasi ya pili baada ya Argentina kuifunga Ufaransa 4-2 kwa mikwaju ya penalti baada ya sare ya 3-3 katika muda wa nyongeza.

"Nous reviendrons," Mbappe alisema. Maana yake, "Tutarudi!"

Mshambuliaji wa Ufranasa  ataondoka Qatar  kama mfungaji bora zaidi wa shindano baada ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao matatu katika fainali ya Kombe la dunia tangu alipofunga mabao hayo  Geoff Hurst  mwaka 1966 -lakini kumbukumbu yake kuu itakuwa ni machungu ya kushindwa. 

 Baada ya mwisho wa mechi ya kusisimua kusema kweli , Mbappe mwenye umri wa miaka 23 bado aliweza kupanda kwenye jukwaa la ushindi kuchukua tuzo lake binafsi baada ya kuionyesha dunia kipaji chake kikubwa katika soka – lakini kulikuwa na kipindi ambapo  ilionekana kuwa alikaribia kupata zawadi kubwa zaidi.   

Hii ingekuwa fainali yake, na kufahamika kama shindano lake pia, lakini kwa yeyote haya yote atakumbukwa mchezaji mwingine nambari 10, ambaye pia alinyenyua Kombe la Dunia, ambalo Mbappe alilipeleka nyumbani miaka minne iliyopita.