Christiano Ronaldo amuondoa mtoto wake Man U na kumpeleka Real Madrid

Mtoto huyo mwenye umri wa miaka 12 amekuwa akichezea kikosi cha vijana wasiozidi umri wa miaka 14 cha Man U.

Muhtasari

• Akichezea U-14 ya Man u, mtoto huyo amefunga mabao 58 kwa mechi 23 na kutoa asisti 18.

• Kuondoka kwake Man U kunakuja siku kadhaa baada ya babake kuvunja mkataba na timu hiyo ya Uingereza.

Christiano ROnaldo akishiriki mazoezi na mwanawe.
Christiano ROnaldo akishiriki mazoezi na mwanawe.
Image: Maktaba

Christiano Ronaldo Jr, mtoto wa staa wa Ureno Christiano Ronaldo ameitema timu ya Manchester United na kujiunga na timu ya vijana wasiozidi umri wa miaka 14 ya Real Madrid.

Mtoto huyo alirejea katika miamba hao wa Uhispania ikiwa ni miaka 4 tangu kuondoka alipomfuata baba yake kwenda Juventus na kisha wakaenda naye Uingereza timu ya Man U.

Hatua ya mtoto huyo kuondoka Manchestr United inakuja mwezi mmoja tangu babake Christiano Ronaldo kuvunjiwa mkataba wake na timu hiyo baada ya mahojiano makali ambapo alito tuhuma za kuichafua na kuidhalilisha Man U.

Kinda huyo wa miaka 12 amekuwa akifuata baba yake na kujiunga na timu ya watoto lakini sasa majarida yanaripoti kuwa Ronaldo ameamua kuvunja kabisa uhusiano na United baada ya kumuondoa mtoto wake klabuni hapo na kumrejesha Real Madrid ambapo pia wiki jana alionekana akishiriki mazoezi huku akiendelea kujinoa kwa kutafuta klabu mpya.

Baba yake alikaa Madrid kwa miaka tisa ambapo aliondoka kama mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo akiwa na mabao 450 na mataji manne ya Ligi ya Mabingwa.

Ronaldo Junior hadi sasa ameweka namba za kuvutia kwenye akademi alizokuwa nazo huku akiiga sherehe maarufu ya baba yake: Siuuu!

Akiwa na umri wa miaka 12 tu Cristiano Jr amekuwa akichezea kikosi cha Manchester United U-14 akifunga magoli 58, Assists 18 katika mechi 23

Christiano ROnaldo akishiriki mazoezi na mwanawe.
Christiano ROnaldo akishiriki mazoezi na mwanawe.
Image: Maktaba