Al Nassr yaongeza wafuasi milioni 2 Instagram chini ya saa 10 tu baada ya kumsaini Ronaldo

Kabla ya kumsaini Ronaldo, timu hiyo ilikuwa na wafuasi 860K lakini saa chache baada ya kumtambulisha Ronaldo, ufuasi wao ulipanda hadi milioni 2.8

Muhtasari

• Itakumbukwa mpaka sasa, Ronaldo ndiye mtu wa kwanza kuwahi kutokea kufikisha wafuasi zaidi ya nusu bilioni kwenye Instagram.

Ronaldo aleta mafanikio makubwa kwenye Instagram ya Al Nassr
Ronaldo aleta mafanikio makubwa kwenye Instagram ya Al Nassr
Image: Instagram

Usiku wa kuamkia Jumamosi, timy ya Al Nassr ilitangaza kumsaini mmoja kati ya wachezaji mastaa maarufu zaidi duniani katika karne hii, Christiano Ronaldo.

Taarifa za kuzipata huduma za mchezaji huyo zilipasua mitandao ya kijamii huku klabu hiyo pamja na mreno Ronaldo wakiwa wanatrend kweney mitandao yote kote duniani.

Athari ya mchezaji huyo kukubali mkataba na Al Nassr tayari zimehisiwa kwa njia chanya na klabu hiyo kwani namba za wafuasi wao kwenye Instagram zimepanda mara dufu na kuvuka mamilioni chini ya saa 10 tu za kutangazwa kwa Roanaldo kuwa mchezaji wao.

Awali kabla ya ujio wa Christian Ronadlo katika uzi wa timu hiyo, ufuasi wao katika mtandao wa Instagram ulikuwa chini ya milioni moja ambapo walikuwa wanajivunia ufuasi wa watu laki 8 na elfu 60.

Lakini chini ya saa 8 tu baada ya kumtambulisha rasmi Ronaldo kama mchezaji wao, wafuasi wa Al Nassr kwenye Instagram wameongezeka hadi milioni 2.8 wakielekea milioni 3 sasa.

 Baadhi wamemsifia Ronaldo kwa kufanikisha hili la ufuasi mkubwa anaojivunia kwenye Instagram na wanahisi kuwa mashabiki wake ndio wameamua kumfuata kwenda timu ya Saudia ili waendelee kushuhudia vimbwanga vyake uwanjani.

Ikumbukwe kuwa mchezaji huyo ndiye anayeshikilia rekodi ya mwanadamu mweney ufuasi mkubwa zaidi kweney mtandao wa Instagram, wafuasi wake wakiwa ni zaidi ya nusu bilioni.