Meikayla Moore: Mchezaji pekee kufunga "Hattrick ya Own-goals" mwaka 2022

New Zealand ilikuwa inacheza na Marekani Februari 2022 ambapo Moore alifanya tukio ambalo halitakuja kusahaulika katika malimwengu ya soka.

Muhtasari

• Baada ya kufunga timu yake kwa 'own goal' ya tatu kunako dakika 36, aliondolewa mchezoni dakika ya 39.

Mchezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya New Zealand
Mchezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya New Zealand
Image: Give Me Sport

Mwaka wa 2022 ulikuwa ni mwaka wenye shughuli nyingi haswa katika tasnia ya spoti si tu katika bara la Afrika bali kote ulimwenguni.

Ndio mwaka ambao bara la Afrika lilishuhudia mashindano yac AFCON nchini Cameroon ambapo Senegali waliibuka washindi.

Mwaka huo pia ulishuhudia mashindano ya kombe la dunia kufanyika kwa mara ya kwanza katika historia katika taifa la Mashariki ya Kati, Qatar ambapo Messi kwa mara ya kwanza aliongoza Argentina kutawazwa mabingwa kwa kuinyuka waliokuwa mabingwa watetezi, Ufaransa.

Lakini pia ndio mwaka ulioshuhudia mchezaji mmoja akifunga mabao matatu almaarufu Hattrick, si kwa timu pinzani kama ilivyo kawaida bali mabao matatu hayo yalifungwa na mchezaji mmoja katika lango la timu yake.

Si uongo, ni kweli, tena kweli kabisa!

Mchezaji Meikayla Moore, anayecheza katika ligi ya New Zealand aliingia katika vitabu vya historia kuwa mchezaji wa kwanza kufunga ‘hattrick’ kwa lango la goli ya timu ambayo alikuwa anaitumikia uwanjani.

Nini kilitokea?

Nyota huyo wa New Zealand Women, ambaye kwa sasa anachezea klabu yake ya Glasgow City, alivumilia wakati mgumu dhidi ya Marekani wakati wa Kombe la SheBelieves mnamo Februari -- akigeuza mpira nyuma ya wavu wa timu yake mara tatu tofauti ndani ya dakika 36.

Katika mechi hiyo ambayo Marekani waliibuka washindi dhidi ya New Zealand mabao 5 kwa nunge, Moore alifunga bao la kwanza la kujifunga wenyewe dakika ya 5, akarejea tena dakika ya sita na kurudia kosa hilo na kumaliza hattrick dakika ya 36 kabla ya kutolewa mchezoni dakika ya 39.