Ronaldo na mkewe hawajaoana rasmi, je wanaweza kuishi Saudia na kuvunja sheria hiyo?

Sheria za taifa hilo hasirihusu wapenzi wawili kuishi pamoja kabla ya ndoa rasmi.

Muhtasari

• Ronaldo na mpenzi wake Georgina Rodriguez wako pamoja lakini hawajafunga ndoa na kwa mujibu wa sheria za Saudia, ni kinyume cha sheria kuishi nyumba moja bila kuoana.

Ronaldo na familia yake wakati wa uzinduzi wake Alc Nassr.
Ronaldo na familia yake wakati wa uzinduzi wake Alc Nassr.
Image: Instagram

Cristiano Ronaldo na mpenzi wake wa siku nyingi Georgina Rodriguez wanakaribia kuvunja sheria kwa kuishi pamoja nchini Saudi Arabia. Ronaldo na Georgina wako pamoja lakini hawajaoana na kwa mujibu wa sheria za Saudia, ni kinyume cha sheria kuishi nyumba moja bila kuoana, lakini hawatarajiwi kuadhibiwa na mamlaka.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 alijiunga na Al-Nassr mwezi uliopita baada ya kuondoka kwake kwa bahati mbaya kutoka Manchester United na inasemekana atalipwa £175m kwa mwaka.

Kulingana na shirika la habari la Uhispania EFE kutokana na hadhi ya Ronaldo kama mmoja wa wanamichezo wanaopigiwa upato zaidi ulimwenguni, nyota huyo wa Ureno hana uwezekano wa kuadhibiwa.

Sheria katika mataifa mengi ya Kiislamu zinazingatia sana suala na ndoa na wawili ambao wanapatikana wakiishi kama mke na mume bila ndoa huchukuliwa hatua kali.

Ronaldo angali bado kufunga ndoa rasmi na mkewe Georgina Rodriguez tangu alipomkuta mwaka 2016 akichezea timu ya Real Madrid.

Alitambulishwa kwa mashabiki siku ya Jumanne alipotambulishwa kama 'mwanasoka bora zaidi duniani' mbele ya wafuasi 25,000 wakali katika uwanja wa Mrsool Park huko Riyadh, baada ya fataki, miali na kuwasha milio.

Familia ya Ronaldo pia ilikuwa uwanjani kwenye uzinduzi wake na jarida la Uhispania la SPORT lilifichua kwamba kwa kuishi na Rodriguez, wawili hao watakuwa wanavunja sheria za Saudia.

Ronaldo alitarajia kucheza kwa mara ya kwanza katika klabu yake hiyo mpya Alhamisi usiku, lakini Sportsmail ilifichua pekee jinsi mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 amepigwa marufuku huku akiwa bado hajatumikia adhabu ya FA kwa mechi mbili kwa kuvunja simu ya shabiki wa Everton msimu uliopita.