Skendo ya upangaji wa matokeo kwa misimu 4 yakumba timu ya Benfica

Skendo hii ilifichuliwa baada ya barua pepe kuvujishwa jinsi Benfica walikuwa wananufaika kutoka kwa uoangaji matokeo kati ya 2016-2020.

Muhtasari

• Taarifa hizo zilifichuliwa na vyombo vya habari vya Ureno kabla ya Benfica yenyewe kutoa taarifa ya kudhibitisha hilo.

• Klabu hiyo ambayo ni miongoni mwa timu kubwa Ureno ilitajwa kufaidika na matokeo ghushi kati ya mwaka 2016 hadi 2020.

Timu ya Benfica
Timu ya Benfica
Image: Twitter

Timu ya Benfica inayoshiriki ligi kuu ya Ureno imejipata pabaya baada ya meseji za barua pepe kuhusu uoangaji wa matokeo kuvujishwa.

Kulingana na jarida la The Sun, klabu hiyo imekuwa ikijihusisha na uhaini wa kupanga matokeo kwa misimu minne mfululizo kati ya mwaka 2016 hadi 2020, sakata hili likiwahusisha viongozi wa timu hiyo kuanzia rais wake.

Kulingana na jarida lac Daily Mail, madai hayo yanakuja mwaka mmoja na nusu baada ya uongozi wa klabu hiyo kukumbwa na mzozo uliopelekea aliyekuwa rais Luis Filipe Vieira kujiuzulu kufuatia kupatikana na hatia ya kukwepa kulipa ushuru, utakatishaji wa fedha pamoja na kughushi.

Baada ya kujiuzulu kwake, lejendari wa timu ya Benfica Rui Costa alichukua hatamu za uongozi kama rais lakini sasa naye amepatikana na skendo kubwa ya upangaji wa matokeo.

Uchunguzi huo unasemekana unatokana na waendesha mashtaka kupata barua pepe, huku klabu hiyo ikidaiwa kunufaika na matokeo kadhaa ya udanganyifu katika kipindi husika cha uchunguzi.

Costa, ambaye hapo awali aliteuliwa kuwa makamu wa rais kwa miaka minne ya 2020-2024 kabla ya kuchukua usukani, ni miongoni mwa viongozi wa klabu hiyo wanaochunguzwa kwa sasa, kulingana na vyombo vya habari vya Ureno.

Taarifa za klabu hiyo kukabiliwa na uchunguzi ziliripotiwa awali kwenye vyombo vya habari vya nchi hiyo kabla ya Benfica kuamua kuthibitisha taarifa hizo.

“Kwa kuzingatia habari zilizotangazwa kwa umma leo, Sport Lisboa e Benfica - Futebol inathibitisha kwamba ilifikishwa mahakamani Januari 3, pamoja na, miongoni mwa wengine, wanachama wa Bodi ya Wakurugenzi kutoka 2016 hadi 2020 na ambao wako katika ofisi,” taarifa fupi ya kampuni inasomeka kulingana na Daily Mail.