Shabiki mtoto ataka kutoa mamake kwa Rashford ili kupata jezi yake

Haitarajiwi kuona Rashford akikubali ombi hili la kuchekesha lakini shabiki huyo mtoto anahitaji kongole kwa ujasiri na udhubutu.

Muhtasari

• “Rashford naeza badilishana mamangu na wewe ili nipate jezi yako,” bango hilo lilisoma.

Shabiki ataka kubadilishana mamake kwa jezi ya Rashford
Shabiki ataka kubadilishana mamake kwa jezi ya Rashford
Image: Twitter, Getty Images

Mshambuliaji wa timu ya Manchester United Marcus Rashford katika siku za hivi karibuni amekuwa akionesha viwango vizuri katika mchezo wake huku akiwa amenfunga mabao sita kwa mechi 6 mfululizo sasa.

Katika mechi yao ya kombe la ngao ya EFL dhidi ya malimbukeni Charlton, Rashford kwa mara nyingine tena aliendeleza rekodi yake nzuri alipofunga mabao mawili na kuiwezesha United kufuzu kwa raondi nyingine kwa kibano cha mabao 3 kapa.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza kwa sasa amefunga mabao 15 msimu huu, huku bao lake la kuvutia lilimfanya aone wavu kwa mechi ya sita mfululizo na mechi ya nane mfululizo Old Trafford.

Fomu hii yake nzuri imevutia mashabiki wengi ambao sasa wanamtazama kama mwokozi wa United.

Shabiki mmoja mtoto aligonga vichwa vya habari alipoonekana amebeba bango lenye ujumbe kwa mchezxaji huyo.

Ujumbe wenyewe ulikuwa wa kuchekesha pale ambapo kijana huyo mdogo alikuwa na ombi la kupata jezi ya Rashford kwa kuweka mamake bondi kwa mchezaji huyo.

“Rashford naeza badilishana mamangu na wewe ili nipate jezi yako,” bango hilo lilisoma.

Marcus Rashford amefunga sasa katika mechi 8 mfululizo za nyumbani akiwa na Manchester United, akiwa mchezaji wa kwanza kufanya hivyo tangu Wayne Rooney mwezi Machi 2010.

Wikendi, United wana kibarua kikubwa dhidi ya mahasimu wao wakubwa Manchester City ambayo itakuwa ni debi la kukata na shoka.

Inasubiriwa kuonwa iwapo Rashford ataendeleza fomu yake nzuri ya kupachika mabao au mabeki wa City watamsoma vizuri na kumdhibiti.