Ronaldo kuishi na familia yake kwa vyumba 17 vya hoteli ya kifahari Saudia

Vyumba hivyo vinatajwa kugharimu shilingi milioni 37 kwa miaka miwili na unusu ya mkataba wake.

Muhtasari

• Ronaldo alikabidhiwa vyumba hivyo 17 ikiwemo makazi yake na familia yake pamoja na wafanyikazi wake wote.

• Ataishi hapo kwa miaka miwili na nusu ambayo ndio aliandikisha kwenye mkataba na timu ya Al Nassr.

Maelezo ya makazi ya Ronaldo Saudia yafichuliwa
Maelezo ya makazi ya Ronaldo Saudia yafichuliwa
Image: fACEBOOK

Mchezaji nyota wa soka Cristiano Ronaldo, ambaye hivi majuzi alisaini mkataba na klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia, anaripotiwa kukaa katika chumba cha kifahari nchini Saudi Arabia. Bado kuchezea klabu yake mpya, Ronaldo anakaa katika Hoteli ya Four Season's Kingdom Suite kwa miaka miwili na nusu ambayo iko kwenye mkataba wake

Nyota huyo wa zamani wa Manchester United, amekuwa akiishi kwenye hoteli hiyo ya kifahari kwa karibia mwezi mmoja tangu aelekee Saudia.

Amewekwa katika moja ya vyumba bora zaidi ambavyo Riyadh inaweza kutoa katika moja ya vyumba 17 vinavyokaliwa na wasaidizi wake, ikiwa ni pamoja na familia yake, walinzi, ripoti ya Daily Mail ilisema.

Iliongeza zaidi kwamba wapishi wanatoa huduma ya kipekee ya chumba cha kulia kwa Ronaldo na familia yake. Zaidi ya hayo, wafanyakazi wametakiwa kutoomba picha za selfie na nyota huyo.

Mchezaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 37 alitia saini mkataba na klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia, ambao unaaminika kuwa na thamani ya zaidi ya euro milioni 200. Mkataba huo wa miaka miwili na nusu utaendelea hadi Juni 2025.

Al Nassr walikuwa wametoa taarifa wakisema mshindi huyo mara tano wa Ballon D’or atajiunga kwa makubaliano hadi 2025 lakini hakufichua maelezo yoyote ya kifedha. Mkataba wa Ronaldo umekadiriwa na vyombo vya habari kuwa na thamani ya zaidi ya milioni €200 milioni (milioni $214.04).