logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Alexis Sanchez awatakia heri Wanabunduki kabla ya mechi dhidi Mashetani Wekundu

Sanchez amewapongeza Arsenal huku wakijiandaa kumenyana na klabu yake nyingine ya zamani, Manchester United.

image
na Radio Jambo

Makala22 January 2023 - 09:02

Muhtasari


•Sanchez aliipongeza Arsenal wakati wanajiandaa kwa mechi kubwa dhidi ya klabu yake nyingine ya zamani Manchester United katika Uwanja wa Emirates siku ya Jumapili jioni.

•Alichukua fursa hiyo kufunguka kuhusu upendo wake kwa klabu hiyo na kuwatakia kila la heri msimu ukiendelea.

amewatakia heri wanabunduki wanapojiandaa kumenyana na United

Mshambulizi wa Chile Alexis Sanchez ameitakia kila la kheri klabu yake ya zamani ya Arsenal katika mashindano ya Ligi Kuu ya Uingereza msimu wa 2022/23.

Sanchez aliipongeza klabu hiyo ya London, Uingereza wakati wanajiandaa kwa mechi kubwa dhidi ya klabu yake nyingine ya zamani Manchester United katika Uwanja wa Emirates siku ya Jumapili jioni.

Kabla ya mchuano huo unaosubiriwa kwa hamu, Wanabunduki walichapisha video ya maktaba ya mshambuliaji huyo  matata akifunga dhidi ya United  katika ushindi wao wa 3-0 takriban miaka minane iliyopita.

"Hakuna kuzuia roketi hiyo ya Alexis," Arsenal waliandika chini ya video ambayo ilichapishwa Jumamosi kwenye Instagram.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34  ni miongoni mwa wanamitandao waliotoa maoni chini ya video hiyo na alishangaa kwamba klabu hiyo ilimkumbuka licha ya uhamisho wake tatanishi kuenda United mwaka wa 2018.

Alichukua fursa hiyo kufunguka kuhusu upendo wake kwa klabu hiyo na kuwatakia kila la heri msimu ukiendelea.

"Mmenikumbuka 😅. Sitawasahau  pia. Mtakuwa moyoni mwangu kila wakati, mlikuwa familia yangu ya kwanza Uingereza, na kila mtu alinitunza vizuri haswa mashabiki! kila la kheri wanabunduki!!" aliandika.

Pia alichapisha video hiyo kwenye ukurasa wake na kuandika ujumbe sawa.

Sanchez alikamilisha uhamisho wake wa kwenda kujiunga na Mashetani Wekundu  mnamo Januari 2018, hatua ambayo iliwaudhi sana mashabiki wa Arsenal kote duniani ikizingatiwa uhasama kati ya vilabu hivyo viwili.

Raia huyo wa Chile hata hivyo hakuwa na wakati mzuri katika United kama aliokuwa nao akiwa na Wanabunduki huku akifichua baadaye kwamba hakuwahi kuhisi kama amekaribishwa katika klabu hiyo ya Manchester.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved