Sajili mpya wa Chelsea Mykhailo Mudryk aweka rekodi ya mchezaji mwenye kasi zaidi EPL

Mudryk alishiriki dakika chache katika mechi ya kwanza dhidi ya Liverpool na kuweka rekodi ya kasi ya 36.63 km/hr

Muhtasari

• Katika orodha ya wachezaji watano bora wenye kasi, Chelsea inajivunia kuwa na wachezaji wawili, Mudryk na Zakaria.

Sajili mpya wa Chelsea Mykhailo Mudryk akiwa mchezoni dhidi ya Liverpool wikendi iliyopita
Sajili mpya wa Chelsea Mykhailo Mudryk akiwa mchezoni dhidi ya Liverpool wikendi iliyopita
Image: Facebook//ESPN, Chelsea

Sajili mpya wa Chelsea Mykhailo Mudryk ameweka rekodi mpya katika ligi kuu ya Premia kama mchezaji mwenye kasi ya juu zaidi kuliko duma.

Ujio mfupi wa Mykhailo Mudryk kwa Chelsea katika mechi dhidi ya Liverpool wikendi iliyopita ulitoa dalili ya mapema kwa nini klabu hiyo ililipa pesa nyingi kwa ajili yake.

Mechi yake ya kwanza ugani Anfield ilionyesha winga wa umeme ambaye atawapa shida nyingi mabeki wa pembeni kwa kasi yake.

Kulingana na jarida la ESPN, Mudryk aliweka rekod mpya yenye kasi ya kilomita 36.63 kwa saa.

“Takwimu rasmi sasa zinaonyesha kuwa Mudryk alihitaji dakika 35 pekee kuvunja rekodi ya Ligi Kuu msimu huu. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 sasa ndiye mchezaji mwenye kasi zaidi katika msimu wa 2022/2023, baada ya kutumia kasi ya 36.63 km/h dhidi ya Reds,” ESPN waliripoti.

Mchezaji huyo ambaye alicheza kwa dakika chache tu sasa ameshikilia nambari ya kwanza na kuwapiku washambuliaji Darwin Nunez na Earling Halaand ambao wamekuwa wakishikilia rekodi hiyo.

Orodha kamili ya wachezaji wenye kasi katika ligi ya premia sasa ni kama ifuatavyo;

1.Mykhailo Mudryk wa Chelsea 36.63km/h

2 Anthony Gordon wa Everton 36.61km/h

3 Darwin Nunez wa Liverpool 36.53km/h

4 Erling Haaland wa Manchester City 36.22 km/h

5 Dennis Zakaria wa Chelsea 36.09km/h