Instastory yasababisha kuvunjika kwa uhusiano wa Gabriel Jesus na mpenzi wake

Jesus mwenye miaka 25 na mpenzi wake Raiane Lima wa miaka 21 walipata mtoto wao wa kike takribani miezi 8 tu iliyopita.

Muhtasari

• Inaarifiwa kuwa Raiane Lima aliandika ujumbe wa kuvinja uchumba kwenye Instagram yake na kuufuta dakika kadhaa baadae.

• Wawili hao wamekuwa pamoja tangu mwaka 2021 na miezi 8 iliyopita walibarikiwa na mtoto wa kike kwa jina Helena.

Gabriel Jesus adaiwa kuachwa na mpenzi wake Raiane Lima
Gabriel Jesus adaiwa kuachwa na mpenzi wake Raiane Lima
Image: Instagram

Mshambuliaji wa Arsenal Mbrazil Gabriel Jesus ameripotiwa kuachwa na mpenzi wake Riaine Lima miezi minane tu baada ya wachumba hao wachanga kukaribisha mtoto wao.

Kulingana na jarida la The Sun la nchini Uingereza, Ripoti nchini Brazil ziliibuka kuwa mshawishi wa mitandao ya kijamii Raiane, 21, alitangaza kuwa ametengana na nyota huyo wa Arsenal, 25, kufuatia hadithi inayodaiwa kuwa kwenye Instagram (Instastory).

Jarida hilo pia lilizidi kufichua kuwa Chombo cha UOL cha Brazil kinadai Raiane alitumia Instagram story yake kuthibitisha habari hizo, lakini chapisho lake halipatikani tena.

Anadaiwa kuandika kwenye instastory yake: "Kabla ya uvumi kuenea, mimi mwenyewe hufanya hatua ya kukujulisha kuwa mimi na Gabriel sio wanandoa tena. Na yeyote anayetaka kuhukumu anaweza kuhukumu. Yeyote anayetaka kusema mambo mabaya anaweza kusema. Kwa kuwa wengine wanapenda fedheha, mimi hufanya hivyo mwenyewe swali la kutangaza mwisho wa kitu ambacho karibu kunimaliza. Nani anataka kusherehekea pia, anaweza kusherehekea (hasa wanafamilia).”

"Baada ya chapisho hili, unajua kuwa hautaniona tena nikizungumza juu ya tuliyopitia, au juu ya somo lolote linalohusiana na binti yetu. Haukuwa usaliti, ilikuwa shinikizo kutoka kwa kila mtu na kila kitu. Tuliishi vizuri, lakini kwa sababu ya shida za watu wengine, kila wakati ilitupata. Siwezi kuvumilia tena, na sitajilazimisha kufanya kitu ambacho kinaniua,” The Sun walinukuu instastory hiyo ambayo ilifutwa baada ya muda mfupi.

Inakuja miezi minane tu baada ya Raiane kujifungua mtoto wao wa kike, Helena. Hakuna picha za Jesus na Raiane wakiwa pamoja kwenye ukurasa wake wa Instagram, kwani inaaminika ameshazifuta zote.

Wapenzi hao wachanga Wanaripotiwa kuwa pamoja tangu Julai 2021.