Ronaldo ashindwa kulenga shuti hata moja langoni Al Nassr ikidhalilishwa nusu fainali

Al Nassr walibanduliwa katika nusu fainali ya Super Cup kwa kibano cha mabao 3-1 Ronaldo akishindwa kupiga shuti hata moja.

Muhtasari

• Mashabiki wa United walifutika mitandaoni kumzomea na kumkejeli huku hii ikiwa mechi yake ya pili bila shuti hata moja langoni.

Al Nassr ya Ronado yavurunda mno
Al Nassr ya Ronado yavurunda mno
Image: Twitter

Mchezaji Christinao Ronaldo alishindwa kuisaidia timu yake mpya ya Al Nassr kufana katika awamu ya nusu fainali ya  mashindano ya Super Cup nchini Saudia Arabia.

Al Nassr ya Cristiano Ronaldo iliondolewa kwenye michuano ya Super Cup ya Saudi Arabia siku ya Alhamisi baada ya kufungwa 3-1 na Al Ittihad kwenye Uwanja wa Kimataifa wa King Fahd.

Fowadi wa Al Ittihad, Romarinho alifunga bao la kwanza dakika ya 15 tu ya mchezo, huku fowadi Hamdallah akiiongezea Al Ittihad bao la pili kabla ya kipindi cha mapumziko.

Al Nassr walipunguza idadi ya mabao kwa bao la kiungo Talisca kipindi cha pili, lakini Al Ittihad wakahitimisha ushindi huo kwa bao la tatu lililofungwa na beki Muhannad Shanqeeti dakika za majeruhi.

Al Ittihad watavaana na Al Feiha katika fainali siku ya Jumapili.

Licha ya kushiriki katika mechi hiyo, Ronaldo alishindwa kusajili shuti hata moja lililolenga lango wakati wa mechi yake ya kwanza, ushindi wa 1-0 dhidi ya Ettifaq, na mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno alishindwa kufanya hivyo tena wakati wa kichapo cha Alhamisi jioni katika nusu fainali ya Kombe la Super Cup la Saudi.

 Itakuwa sawa kusema umekuwa mwanzo mgumu kwa mkongwe huyo, na wafuasi wa Reds walienda kwenye Twitter baada ya habari hiyo kuchangia mawazo yao.