Chelsea wamtambua kocha mpya wa kuchukua nafasi ya Graham Potter

Tangu mwezi Desemba, ligi ya Premia iliporejea, Chelsea hawajakuwa wakipata matokeo ya kufurahisha.

Muhtasari

• Taarifa hizi zinajiri wakati ambapo kumekuwa na uvumi kuwa Mourinho anamezea nafasi ya kurejea London kwa mara ya tatu kuifunza Chelsea.

Raia wa Austria Oliver Glasner
Raia wa Austria Oliver Glasner
Image: Twitter

Unaambiwa safari ya kesho huandaliwa leo.

Majarida mbalimbali barani Uropa yanaripoti kuwa klabu ya Chelsea imeanzisha mipango ya kumpata kocha mpya endapo watamfuta kazi Muingereza Graham Potter, jambo ambalo uwezekano wake ni mkubwa.

Kulingana na Jarida la The Sun, Chelsea tayari wameweka wazi kuwa watamuajiri kocha mkuu wa timu ya Eintracht Frankfurt ya Ujerumani Oliver Glasner ambaye aliisaidia timu hiyo ya Bundesliga msimu uliopita kubebqa ubingwa wa ligi ya Uropa.

Ushindi wa hivi punde zaidi wa Glasner ulikuja na sare ya 1-1 dhidi ya mabingwa wa kudumu wa Ujerumani Bayern Munich.

Na jarida la Bild linadai kuwa mtaalamu huyo wa Austria anashabikiwa pakubwa na mmiliki wa Chelsea Todd Boehly.

Inasemekana kuwa The Blues waliwasiliana na Glasner msimu uliopita wa joto wakati mustakabali wa Thomas Tuchel ulipoangaziwa.

Na anaendelea kuwa kwenye orodha fupi ya Boehly iwapo atawahi kuamua kumpiga kalamu Potter.

Mkufunzi huyo wa zamani wa Brighton alianza vyema Stamford Bridge kabla ya matokeo duni kushuhudiwa Chelsea. Lakini kuna hali ya kujisikia vizuri katika klabu baada ya matokeo mazuri na utitiri wa vipaji vya hali ya juu.

Chelsea pia bado wako kwenye Ligi ya Mabingwa na mashabiki wanaamini kwamba njia pekee ni wanawinda kiungo mpya wa kati kabla ya tarehe ya mwisho ya Jumanne.

Timu hiyo tangu kurejelewa kwa michezo ya ligi ya Premia baada ya likizo fupi ya kuoisha mashindano ya kombe la dunia, haijakuwa na matokeo mazuri huku mpaka sasa wakiwa katika nafasi ya kumi, nje ya kushiriki kombe la ubingwa wa Uropa, ligi ya uropa na hata kombe la conference.

Lakini huku Mmarekani huyo akimmezea macho Glasner, Potter atafahamu kwamba lazima aanze kupata ushindi chini ya mkanda wake, haswa katika Ligi ya Premia.

Kuvutiwa kwa Chelsea kwa Glasner kunakuja baada ya Jose Mourinho kuhusishwa na kurejea kwa kipindi cha TATU.

Kocha huyo wa sasa wa Roma ameiongoza Man Utd na Tottenham tangu alipotimuliwa kwa mara ya pili Chelsea Desemba 2015.