Mchezaji wa Roma kuichukua hatua za kisheria klabu hiyo kwa kumtishia maisha

Zogo lilianza wakati mchezaji huyo alikataa kuihama timu hiyo licha ya timu kufikia makubaliano kumuuza kwenda timu nyingine.

Muhtasari

• Mchezaji huyo wa Kiitaliano alikuwa karibu na kuondoka kwenye Serie A baada ya kikosi cha Jose Mourinho kufikia makubaliano ya pauni milioni 30 na Bournemouth wiki iliyopita.

Nicvolo Zaniola wa Roma kuishtaki klabu hiyo kwa kumtishia maisha
Nicvolo Zaniola wa Roma kuishtaki klabu hiyo kwa kumtishia maisha
Image: Twitter

Nicolo Zaniolo, Winga wa timu ya AS Roma inayoshiriki katika ligi ya Italia Serie A ana mpango wa kuwashtaki Roma kwa 'shinikizo la kisaikolojia na kuwashawishi' katika kipindi chote cha uhamisho wa Januari, kulingana na ripoti.

Inadaiwa kwamba Zaniola alipokea vitisho vya maisha kutoka kwa watu ndani ya klabu hiyo wakiwemo mashabiki baada ya kukataa kuuzwa katika kipindi cha dirisha la uhamisho Januari.

Mchezaji huyo wa Kiitaliano alikuwa karibu na kuondoka kwenye Serie A baada ya kikosi cha Jose Mourinho kufikia makubaliano ya pauni milioni 30 na Bournemouth wiki iliyopita.

Awali Zaniolo alikataa hatua hiyo lakini alionekana kubadili mawazo yake siku moja baadaye, hata hivyo Cherries ndio ambao hatimaye walirudi nyuma kwenye mpango huo kutokana na matatizo ya kifedha, Daily Mail Walisema.

Familia ya Zaniolo inadai kwamba 'matamshi ya hivi majuzi ya vyombo vya habari' dhidi ya Muitaliano huyo yamechochewa na klabu.

“Baada ya habari kusambaa kuhusu tamaa ya Zaniolo kuondoka klabuni hapo kwenye dirisha la usajili la Januari, winga huyo alipokea vitisho vya kuuawa na kulazimika kupiga simu polisi baada ya mashabiki wa Roma waliokuwa na hasira kujitokeza nyumbani kwake,” Mail walisema.

Klabu hiyo ilimpa ruhusa ya kusafiri hadi La Spezia na familia yake kwa saa 48 wakati mazungumzo yakiendelea.

Pia wanaripoti kuwa timu ya mawakili wamewasiliana kushughulikia suala hilo. Assocalciatori, ambao wana jukumu la kusaidia wachezaji katika migogoro na vilabu vyao, pia wamearifiwa.

Inaeleweka kuwa Zaniolo atamsubiri Tiago Pinto - mkurugenzi wa michezo wa Roma - kuhudhuria mkutano wake na waandishi wa habari ulioratibiwa kabla ya kutoa maoni juu ya hali hiyo.