Rashford apigwa faini ya Ksh 87k kwa kuendesha Mercedes ya Ksh 102m kwa kasi

Inaarifiwa mchezaji huyo baadae aliuza gari hilo kwa nusu bei na kununua lingine lenye thamani kubwa.

Muhtasari

• Staa huyo wa umri wa miaka 25, alikuwa nyuma ya gurudumu la gari lake aina ya Mercedes G VRM.

Rashford alamba faini
Rashford alamba faini
Image: Twitter

Mshambulizi wa Manchester United, Marcus Rashford amepigwa faini na kupewa pointi za adhabu kwenye leseni yake ya kuendesha gari baada ya kukiri kuendesha gari kwa kasi jijini Manchester mwaka jana.

Mshambulizi huyo wa Manchester United, 25, alikuwa akiendesha gari katikati mwa jiji alipovuka kikomo cha maili 20 kwa saa. Tukio hilo lilitokea Mei 2022 na Rashford alikiri kosa hilo, na kusababisha Mahakama ya Manchester kumpa faini ya pauni 574 sawa na shilingi elfu themanini na saba za Kenya, kwa mujibu wa The Sun. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza pia amepewa pointi sita za penalti kwenye leseni yake.

Staa huyo wa umri wa miaka 25, alikuwa nyuma ya gurudumu la gari lake aina ya Mercedes G VRM katikati mwa jiji la Manchester alipovuka kikomo cha 20mph.

Kulingana na Jarida la The Sun, Rashford alikuwa analiendesha gari lake la kifahari lenye thamani ya shilingi milioni 102 pesa za Kenya.

Mwezi uliopita ilibainika kuwa aliuza gari lake aina ya Mercedes baada ya kuonekana lipo sokoni kwa nusu ya pauni 670,000, sawa na milioni 51 pesa za Kenya alizolipia.

The Sun wanaripoti kuwa alikuwa akiendesha gari hilo la kifahari mara kwa mara hadi kwenye uwanja wa mazoezi wa Manchester United huko Carrington.

Rashford hivi majuzi alimwaga zaidi ya pauni 280,000 kwenye gari la kifahari la McLaren 765 Long Tail na Beji Nyeusi ya Pauni 390,000 Cullinan Rolls Royce.

Inakuja baada ya nyota huyo wa Uingereza kufunga bao lake la 11 la Ligi Kuu ya Uingereza juzi dhidi ya Leeds. Rashford sasa ameifungia Utd mabao 20 kwa jumla msimu huu katika michuano yote. Ina maana mshambuliaji huyo sasa amefunga katika mechi sita mfululizo za Ligi Kuu ya Uingereza.