(Video) Lukaku anaswa kwenye kamera akimtukana mchezaji mwenza uwanjani

Katika video hiyo, Lukaku anaonekana akimnyooshea kidole kwa ukali mchezaji mwenzake baada ya pasi yake kuenda fyongo.

Muhtasari

• Jarida hilo liliripoti kuwa Lukaku alipandwa na hasira baada ya Barella kutokamilisha pasi na badala ya kuifuata, akatupa mikono juu.

Kulikuwa na mzozo mkali kati ya mchezaji Romelu Lukaku na mwenzake Nicolo Barella wakati wa mchezo wa jioni ya Jumatatu kati ya Inter Mlan dhidi ya Sampdoria.

Kulingana na jarida la michezo la Football Italia, Bado ilikuwa bila bao baada ya dakika 40 wakati pasi ilipokoseshwa katikati ya uwanja na Barella alipunga mkono kwa kufadhaika.

Hii si tabia mpya, mara nyingi anafanya hivyo na amekosolewa hapo awali, lakini wakati huu iligonga kwa mtu asiyejali, Football Italia walisema.

Lukaku alinaswa kwenye kamera kwa uwazi kabisa akimfokea Barella na kumpungia kidole.

"Usifanye hivyo, inatosha kwa mikono hii! Usifanye hivyo! Sio nzuri, ni matusi, sasa acha!” jarida hilo lilinukuu.

Barella lazima alisema kitu kibaya wakati wa kujibu, kwa sababu klipu hiyo iliishia kwa Lukaku kusema: "f*** wewe, mtoto wa mbwa!" jarida la Football Italia liliripoti.

Mashabiki wengi mtandaoni waliona majibizano hayo na walikuwa nyuma ya Lukaku, kwa sababu Barella amepata sifa ya kudhihirisha hasira zake kwa wachezaji wenzake badala ya kuwahimiza waendelee.

"Ni jambo la kwanza nzuri ambalo Lukaku amefanya msimu huu," aliandika mfuasi mmoja.

Lukaku alirejea Inter misimu miwili iliyopita kutoka Chelsea kama mchezaji wa mkopo baada ya Chelsea kumnunua kutoka mabingwa hao wa Italia.