Siku 10 sasa, Aliyekuwa mchezaji wa Chelsea hajapatikana kwenye maporomoko Uturuki

Wakala wa mchezaji huo alisema msako dhidi yake kwenye vifusi unaendelea na tayari viatu alivyokuwa anavitumia vimeppatikana.

Muhtasari

• Mpaka sasa, watu zaidi ya elfu 25 wameripotiwa kufariki katika mkasa huo ambao Uturuki na Syria zilitaja kama janga ambalo linahitaji msaada wa jamii za kimataifa.

Christian Atsu, aliyekuwa mchezaji wa Chelsea.
Christian Atsu, aliyekuwa mchezaji wa Chelsea.
Image: Twitter

Aliyekuwa mchezaji wa Chelsea Christian Atsu bado hajapatikana, siku 10 tangu tetemeko kali ligonge nchi za Uturuki na Syria, Wakala wake amefichua.

Atsu, ambaye alikuwa anachezea timu ya Uturuki ya Hatayspor ni miongoni mwa maelfu ya watu ambao walizikwa kwenye vifusi baada ya majengo walimokuwa wakiishi kuporomojka kufuatia zilizala hiyo ya Februari 6.

Ripoti za awali zilidai kuwa Atsu alitolewa kwenye mabaki hayo, lakini daktari wa Hataysor Gurbey Kahveci na wakala Nana Sechere walisema bado hajapatikana.

Sechere alisema Jumanne kwamba kijana huyo mwenye umri wa miaka 31 bado hayupo, lakini jozi mbili za viatu vyake zimegunduliwa.

Katika ukurasa wake wa Twitter, alisema: "Imekuwa siku tisa tangu tetemeko la ardhi na bado hatujapata Atsu. Niko kwenye eneo la tetemeko huko Hatay na familia ya Christian. Matukio hayawezi kufikiria na mioyo yetu imevunjika kwa watu wote walioathiriwa. Wakati nikiwa hapa tumeweza kupata eneo hususa la chumba cha Christian Atsu, na tumepata jozi mbili za viatu vyake.”

"Jana tulipata uthibitisho kwamba picha za joto zinaonyesha dalili za hadi watu 5, hata hivyo, nimeambiwa kuwa uthibitisho wa kweli wa maisha ni kupitia kuona, kunusa na sauti, na kwa bahati mbaya hatukuweza kumpata Atsu.”

"Hii ni hali ngumu na tunashukuru sana timu zote za uokoaji za Uturuki na nje, raia wa ndani na watu waliojitolea kwa juhudi na mwitikio wao katika kuwaokoa manusura. Hata hivyo, tunahitaji rasilimali zaidi kwa haraka, ikiwa ni pamoja na mfasiri, mashinani.”

 

"Mambo yanaenda polepole sana na matokeo yake uokoaji mwingi unacheleweshwa, na maisha yanapotea kwa sababu ya ukosefu wa rasilimali zinazopatikana kwa wafanyikazi. Inasikitisha kwamba klabu haipo uwanjani nasi, bega kwa bega, katika kumtafuta Atsu,” wakala huyo alilalama.

Atsu alijiunga na Hatayspor kwa mkataba wa awali wa mwaka mmoja msimu uliopita baada ya kucheza huko Porto, Chelsea na Newcastle.