Mbappe yuko mbioni kwenda Man U? Insta yatafsiri chapisho lake, Rashford atia neno!

Mbappe alipakia picha yake Instagram na kuandika maneno kwa lugha ya kifaransa lakini Instagram ikayatafsi kwa kizungu kwa kurejelea Man U.

Muhtasari

• Sintofahamu ya Mbappe inakuja wakati ambapo kampuni ya Qatar inayomiliki PSG ya Mbappe inahusishwa kuunganishi mkwasi mmoja kuinunua Man U.

Mbappe atafsiriwa vibaya na Instagram kuhusu Man U.
Mbappe atafsiriwa vibaya na Instagram kuhusu Man U.
Image: Maktaba, Instagram

Kylian Mbappe ameibua sintofahamu kwa kuandika nukuu yake ya hivi punde kwenye Instagram, haswa mashabiki wa Manchester United.

Mbappe alichapisha picha yake akirejea uwanjani kutokana na jeraha wakati wa mechi ya Jumanne ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Bayern Munich, ambayo timu yake ilipoteza kwa bao 1-0 licha ya matokeo yake ya kuvutia.

Lakini ni maelezo yaliyowaacha wengi wakiwa wamechanganyikiwa.

Mbappe alikuwa ameandika kwa lugha ya Kifaransa. Hata hivyo, unapobofya kitufe cha kutafsiri kwenye Instagram inabadilika na kuwa 'timu ya Manchester United sasa iko kwenye PSG.'

Kwa kawaida mashabiki wa United walifurahi kuona mmoja wa wachezaji bora zaidi duniani akionekana kuwataja na Marcus Rashford kisha akaongeza hamaki kwa kuacha emoji ya moto.

Tafsiri hiyo ya ajabu imekuja siku chache tu baada ya habari kusambaa kuwa Mashetani Wekundu hao ambao wamewekwa kuuzwa na familia ya Glazer wanatarajiwa kuwekewa dau la pauni bilioni 4.5 kutoka mfuko wa uwekezaji wa Qatar unaoongozwa na Emir wa Qatar, Sheikh. Tamim bin Hamad al-Thani, Daily mail Online walisema.

Al-Thani alihudhuria mchezo wa Jumanne jijini Paris na ana uhusiano wa moja kwa moja na PSG, kwani klabu hiyo inamilikiwa na shirika alilolianzisha mwaka 2005, Qatar Sports Investments (QSI).

Inasemekana sasa anaongoza juhudi za kuinunua United kabla ya tarehe ya mwisho ya Ijumaa kuwasilisha mapendekezo yake, huku shirika lingine lake - Mamlaka ya Uwekezaji ya Qatar (QIA), ikiaminika kuwa mfadhili wa kifedha.