Arsenal na Man U zina milima ya kukwea katika Europa League, dhidi ya Sporting Lisbon na Real Betis mtawalia

Washindi wa makundi ya Ligi ya Europa walipangwa dhidi ya vilabu vinane vilivyopitia mechi za raundi ya muondoano.

Muhtasari

• United iliwashinda vinara wa La Liga 2-1 kwenye Uwanja wa Old Trafford siku ya Alhamisi na kusajili ushindi wa jumla ya mabao 4-3 katika mechi ya maondoano. 

Manchester United itacheza dhidi ya Real Betis katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Europa baada ya kuifunga Barcelona, ​​huku Arsenal ikimenyana na Sporting Lisbon. 

United iliwashinda vinara wa La Liga 2-1 kwenye Uwanja wa Old Trafford siku ya Alhamisi na kusajili ushindi wa jumla ya mabao 4-3 katika mechi ya maondoano. 

Arsenal watacheza mechi ya mkondo wa pili wa mchujo wao nyumbani baada ya kufuzu kama washindi wa kundi, huku Manchester United wakiwakaribisha Betis katika uwanja wa Old Trafford katika mechi ya mkondo wa kwanza.Mechi za hatua ya 16 bora ya Ligi ya Europa zitafanyika tarehe 9 na 16 Machi. 

Vinara wa Ligi ya Premia Arsenal waliepuka hatua ya mtoano kwa kuongoza Kundi A kwa kushinda mara tano katika mechi zao sita. Sporting, inayoshika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu ya Ureno, iliishinda klabu ya Midtjylland ya Denmark mabao 5-1 katika mechi ya mchujo baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu katika kundi lao la Ligi ya Mabingwa. 

Wakati huohuo, Real Betis inayonolewa na Manuel Pellegrini iko katika nafasi ya tano kwenye La Liga na ilimaliza hatua ya makundi ya Ligi ya Europa ikiwa na rekodi bora zaidi kwenye michuano hiyo, ikishinda tano na kutoka sare moja kati ya mechi zao. Kwingineko, washindi mara sita Sevilla wanakutana na Fenerbahce, huku Roma ya Jose Mourinho ikicheza na Real Sociedad - walioongoza kundi la Manchester United. 

Washindi wanane wa makundi ya Ligi ya Europa walipangwa dhidi ya vilabu vinane vilivyopitia mechi za raundi ya muondoano, vilabu vya shirikisho moja haviruhusiwi kumenyana.

Droo ya awamu ya 16

- Union Berlin v Union Saint-Gilloise

- Sevilla v Fenerbahce

- Juventus v Freiburg

- Bayer Leverkusen v Ferencvaros

- Sporting Lisbon v Arsenal

- Manchester United v Real Betis

- Roma v Real Sociedad

- Shakhtar Donetsk v Feyenoord