Ronaldo kupewa medali baada ya Man U kushinda taji, licha ya kutoshiriki mechi

Mchezaji huyo aliondoka United mwezi Novemba mwaka jana baada ya mahojiano ya mlipuko.

Muhtasari

• Kanuni za EFL zinahoji kwamba timu inayoshinda inapewa medali 30 za kupeana japo United walitumia wachezaji 27 pekee.

• Hiyo ina maana kwamba bado kuna medali 3 ambazo zimebaki na ambazo zinaweza tolewa kwa wachezaji wao waliooondoka katikati ya msimu.

Ronaldo kuppewa medali ya dhahabu kwa ushindi wa United
Ronaldo kuppewa medali ya dhahabu kwa ushindi wa United
Image: Tiwtter

Manchester United wanaweza kumpa Cristiano Ronaldo medali ya mshindi wa Kombe la Carabao baada ya kuwalaza Newcastle 2-0 kwenye fainali siku ya Jumapili, majarida ya Uingereza yameripoti.

United ilichukua kombe la kwanza la utawala wa Erik ten Hag, na la kwanza kwa klabu hiyo katika kipindi cha miaka sita, shukrani kwa mabao ya Casemiro na Marcus Rashford.

Ronaldo aliondoka Old Trafford mwezi Novemba kufuatia mahojiano ya mlipuko ambayo yalimwona akiikosoa klabu hiyo waziwazi.

Itawezekanaje Ronaldo kupewa medali ya dhahabu licha ya kutoshiriki mechi ya Carabao hata moja?

Hakushiriki Kombe la Ligi msimu huu huku kukiwa na uhusiano mbaya na Ten Hag, lakini bado anaweza kuwa kwenye mstari wa kupata medali ya mshindi kupitia kanuni za EFL.

United wana haki ya kupata ' zawadi za medali' 30 kwa kushinda michuano hiyo, lakini walitumia wachezaji 27 pekee katika michezo yao sita, kumaanisha wana tatu za kuwatunuku wachezaji ambao hawakushiriki kama watataka.

Ronaldo, ambaye alishinda mataji mawili ya Ligi katika kipindi chake cha kwanza akiwa United, anaweza kuwa kwenye mstari wa kutwaa medali, ingawa inaonekana si rahisi kutokana na kuondolewa kwake katika klabu hiyo vibaya.

 

Alihamia upande wa Saudi wa Al-Nassr muda mfupi baadaye, ambapo alisaini kwa pesa nyingi. Mkataba wa £175m kwa mwaka.