Wakitumia pesa kidogo watashinda mataji ya maana - Pep akejeli Man U kushinda Carabao

"Ila kwa sasa wako katika nafasi ambayo wanastahili kuwa kawaida," Guardiola alinukuliwa na Metro UK.

Muhtasari

• Mpaka sasa United wako nafasi ya 3 kwenye msimamo wa jedwali la EPL pointi 8 tu nyuma ya vinara Arsenal.

Pep akejeli United kushinda Carabao.
Pep akejeli United kushinda Carabao.
Image: Twitter

Mkufunzi wa timu ya Manchester City Pep Guardiola amekejeli ushindi wa majirani wao Manchester United katika taji la Carabao wikenid iliyopita.

Kulingana na jarida la Metro, Guardiola alikuwa akiulizwa uwezekano wa Manchester United kushinda mataji mengine msimu huu.

Jarida hilo lilikuwa limeripoti kuwa baada ya United kushinda Carabao na kukata kiu ya mataji kwa muda wa miaka 6 iliyopita, bado kikosi cha kocha Eric Ten Hag kimesalia katika mbio za ubingwa wa mataji mengine matatu yakiwemo ligi kuu ya premia, ligi ya Uropa na pia kombe la FA.

Lakini jibu la Guardiola lilichukuliwa na wengi kama kejeli ambapo alisema kuwa United wana uwezo wa kushinda mataji makubwa tena ya maana endapo watakoma kuwa bahili na badala yake kutumia pesa kufanya sajili za maana.

“Ikiwa wanatumia pesa kidogo zaidi, ndiyo, kwa sababu hawakutumia, sivyo? Wako katika nafasi ambayo kwa kawaida wanapaswa kuwa,” Guardiola alinukuliwa na Metro UK.

United ndio timu ya pekee mpaka sasa kwenye EPL ambayo inaonekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kutia kibindoni mataji manne mwishoni mwa msimu huu.

Katika msimamo wa jedwali la EPL, United wameachwa na pointi 8 tu na viongozi wa jedwali, Arsenal, wadadisi wakihisi kuwa katika mechi ambazo zimesalia kukamilisha msimu huu, uwezekano upo kwa United kuipiku Arsenal kileleni.