Neymar aapa kurejea PSG akiwa kwa kishindo zaidi

Mchezaji Neymar aliumia kwenye kifundo cha mguu.

Muhtasari

Paris Saint Germain  ilidhibitisha kuwa Neymar anahitaji upasuaji wa kiundo cha mguu na atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi tatu au minne

Image: BBC

Mchezaji kutoka Brazil,Neymar ambaye anachezea timu ya PSG ,aliahidi kurejea mwenye nguvu zaidi.Hii ni baada ya mchezaji huyo  kuumia kifundo cha mguu mnamo Februari 19 dhidi ya Lille kwenye Ligue 1. Klabu hiyo ilisema kuwa madaktari wake walipendekeza upasuaji wa kurekebisha ligament ili kurekebisha tukio hilo kujirudia .

Timu hiyo iliongeza kuwa Neymar atakuwa nje ya uwanja kwa miezi mitatu hadi minne hivyo uwezekano wa yeye  kuwa kwenye ligi  msimu hii ni kidogo sana kwa sababu  mwisho wa msimu huu utakuwa Juni 3.

"Nitarudi na nguvu zaidi,"alichapisha kwenye mtandao wa Twitter.

Neymar ambaye amefunga mabao 18 katika michuano yote kwa klabu ya msimu huu, alikuwa katika kiwango kizuri kwa mabingwa hao wa Ufaransa kabla ya mapumziko ya Kombe la Dunia .

Lakini mchezaji huyo wa miaka 31 ametikisa nyavu mara tatu pekee katika mechi tisa tangu arejee kutoka Qatar,ambako aliumia kifundo cha mguu akiichezea Brazil.Mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona alirejea katika raundi ya mtoano lakini Brazil wakshindwa na Croatia kwa mikwaju ya penalti katika robo fainali,licha ya Neymar kuwaweka mbele katika  muda wa ziada katika mchezo huu.

Neymar ameweka mabao 118 katika michezo 173 kule aPSG lakini alikosa zaidi ya michezo 100 kwa sababu ya kuumia .Katika Ligue 1 amecheza asilimia 49 pekee ya mechi za PSG ya Ligue 1(112 kati ya 228)