Malalamiko baada ya Shabiki wa kiume kuingia choo za kike akidai ana jinsia mbili

Shabiki huyo sugu wa klabu ya Portsmouth mwenye miaka 59 aliingia choo za kike kwa fujo akidai ana jinsia mbili tofauti.

Muhtasari

• The News inaelewa kuwa Bw Westwood, 59, aliingia kwenye vyoo vya wanawake wakati wa mapumziko.

Shabiki Westwood wa Portsmouth.
Shabiki Westwood wa Portsmouth.
Image: Portsmouth FC

Malalamiko yametumwa kwa klabu ya Portsmouth FC baada ya shabiki maarufu John Westwood kuripotiwa kuingia kwenye vyoo vya wanawake - akidai alikuwa amebadili jinsia.

Kulingana na taarifa kutoka nchini Uingereza, Mashabiki kadhaa wamewasiliana na klabu na Mkurugenzi Mtendaji Andrew Cullen. The News inaelewa kuwa Bw Westwood, 59, aliingia kwenye vyoo vya wanawake wakati wa mapumziko wakati wa kushindwa kwa 1-0 na Sheffield Wednesday Jumamosi.

Inasemekana alitakiwa kuondoka Fratton Park kufuatia tukio hilo. Mmiliki huyo wa tikiti ya msimu anasemekana kuondoka uwanjani kwa hiari yake mwenyewe.

Bwana Westwood amepigwa marufuku mara tatu msimu huu.

Alilaumu ‘kughairi utamaduni’ kwa adhabu ya kwanza baada ya kutoa ishara chafu kwa wafuasi wa Coventry City wakati wa mechi ya kirafiki mwezi Julai.

Bw Westwood pia alipigwa marufuku kwa kukojoa ukuta nje ya uwanja wa Forest Green Rovers na baada ya ishara ya kengele kunaswa na kamera.

Tukio hili linajiri wakati ambapo mitandaoni pia kuna gumzo kubwa kufuatia klipu inayoonesha mchezaji wa Sunderland Luke O’Nien akimpiga busu mchezaji wa Norwich  wakati wa kabiliano la wikendi katika mechi ambayo Sunderland walishinda moja kwa nunge.